HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 1 December 2020

RC KUNENGE AWATAKA WANANCHI KUFANYA USAFI KILA JUMAMOSI YA WIKI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha kila Jumamos wanafanya zoezi la usafi wa mazingira kuanzia saa 12 Asubuhi hadi saa tatu ili kujikinga na magonjwa ya Mlipuko na kuliweka jiji kuwa Safi.

RC Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati alipokuwa anazungumzia zoezi la usafi linalotaraji kufanyika Jumamosi ya Disemba 05 ambapo amesema Mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha magari ya kubeba taka yanakuwa ya kutosha kwenye kila maeneo.

Aidha RC Kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya za Jiji hilo kuhakikisha wanasimamia usafi Katika maeneo yao na kuhakikisha suala la usafi linazingatiwa na kila mmoja.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha suala la usafi linakuwa sehemu ya maisha yao na sio kusubiri kushurutishwa na Sheria.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad