Ondoeni kabisa tabia ya kutengeneza makundi- Tabia - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 10, 2020

Ondoeni kabisa tabia ya kutengeneza makundi- Tabia

 

WAZIRI wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameutaka uongozi wa shirikisho la soka Zanzibar (ZFF) kuacha tabia ya kutengeneza makundi ili kuepuka kuwafarakanisha wachezaji na kusababisha migogoro katika vilabu vya soka hilo. 

 "Ondoeni kabisa tabia ya kutengeneza makundi yatavunja sana..." 

Amesema suala hilo ni chachu ya kujenga chuki na migongano baina yao hali inayopelekea shirikisho la soka Zanzibar kushuka na kuiweka nchi katika nafasi mbaya kisoka. 

Amewasisitiza sana suala la kufuata katiba na kanuni zilizoundwa katika kuendesha shughuli zote za mpira wa miguu ili kuepusha kufanya maamuzi ya ubaguzi, upendeleo na kupelekea sitonfahamu kwa uongozi wa ZFF na vilabu vya mpira.

 Kwa upande mwengine amewasisitiza kuaminiana, kupendana, kushirikiana, kujielewa na kuwajibika ipasavyo ili kuweza kufanikiwa kurejesha haiba ya soka la Zanzibar Aidha Mhe. Tabia ameahidi kushirikiana nao kikamilifu kwa ushauri, kutafuta wadhamini, kupanga na kutekeleza mikakati itakayokuza soka la Zanzibar.

Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (Zanzibar), Tabia Mwita  akizungumza wakati akiteua uongozi wa shirikisho la soka Zanzibar (ZFF) leo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad