Ni Wiki Nyingine ya Soka Safi Barani Ulaya, ‘Derby Weekend’ - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 11 December 2020

Ni Wiki Nyingine ya Soka Safi Barani Ulaya, ‘Derby Weekend’

 *Ndio, hapa Manchester Derby kule Madrid Derby!


Ikiwa ni Wiki ya 11 kunako EPL. Michezo ya majirani ‘derby’ inaendelea kunogesha soka la Uingereza. Baada ya London Derby kwa wiki mbili mfululizo, tunahamia kwenye Manchester Derby wikiendi hii!

Manchester United kuwakaribisha majirani zao Manchester City katika dimba la Old Trafford. Unaambiwa hakuna mchezo unaoibua hisia za mashabiki wa jiji la Manchester kama ‘Manchester Derby’! Hapa utaona mchezo wenye ufundi na upinzani wa hali ya juu. Waswahili wanasema ‘mtoto hatumwi dukani’ wakati mchezo huu unapochezwa.

Turudi nyuma kidogo, msimu uliopita – Man City waliambulia vipigo nje ndani dhidi ya Man United. City alipigwa 2-0 Old Trafford na akaenda kupigwa 2-1 pale Etihad.

Hakika Pep Guardiola ataiongoza City yenye lengo la kulipa kisasi msimu huu. Upande wa pili, United wanamachungu ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na sasa watacheza Ligi ya Europa.

Kwa siku za karibuni, United wamepewa jina la ‘The Come Back Kings’ hii ni baada ya kupindua matokeo katika mechi 2 mfululizo – dhidi ya Southampton na West Ham United. Almanusura wapindue matokeo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa lakini ilishindikana na wakafungwa 3-2.

Je, msimu huu United ataendeleza ubabe wake dhidi ya City kama alivyofanya msimu uliopita au Pep atakataa utumwa? 

Kwa sasa, United inashika nafasi ya 6 huku City wakiwa nafasi ya 7 kwenye msimamo wa EPL.

Turuke kidogo mpaka Hispania kwenye La Liga Sentander. Huku kuna mtanange wa Madrid Derby. Real Madrid kupambana na majirani zao – Atletico Madrid.

Jiji la Madrid huzizima kwa dakika 90 timu hizi zinapokutana uwanjani. Hapa ni soka la viwango linalochagizwa na upinzani wa kimfumo wa uchezaji. 

Atletico ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wa La Liga mpaka sasa wakati ambapo Real Madrid bado hawaeleweki wapo katika kiwango gani, vijana wa Zidane wanamatokeo ya kupanda na kushuka.

Msimu uliopita walitoka sare pale Wanda Metropolitano (0-0) lakini mambo yalikuwa tofauti pale Santiago BernabeuReal Madrid alishinda 1-0. Msimu huu mambo yatakuaje pale Alfredo De Stefano

Kwa sasa, Atletico anaongoza msimamo wa La Liga huku majirani zao – Real Madrid wakiwa nafasi ya 4.

Mchongo mzima upo Meridianbet. Wataalamu wa Meridianbet wamekuwekea odds za michezo hii hapa.  

6 comments:

Post Bottom Ad