MTATIRO AKABIDHI MAMILIONI YALIYOPORWA KWA MSTAAFU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 7, 2020

MTATIRO AKABIDHI MAMILIONI YALIYOPORWA KWA MSTAAFU

 


Taasisi tatu za ukopeshaji wa fedha wilayani Tunduru zimemtapeli Mwalimu Mstaafu Kanyinga Abdallah zaidi ya shilingi milioni 50.

Mwalimu huyo alikopa jumla ya shilingi milioni 10,350,000/- kwenye taasisi tatu tofauti za ukopeshaji fedha wilayani Tunduru, lakini ndani ya mwaka mmoja alipopata pensheni yake taasisi hizo zikampora jumla ya shilingi milioni 59 ikiwemo pesa walizomkopesha na riba ya wastani wa asilimia 600 hadi 1,000.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Tunduru Jumapili ya leo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amemkabidhi mzee huyo ambaye ni mwalimu mstaafu, kiasi cha shilingi milioni 7 ambazo zimerejeshwa na taasisi hizo ambazo zinapaswa kurejesha kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 52 ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2020.

Mtatiro amempongeza sana Kamanda wa TAKUKURU wilayani Tunduru kwa kutekeleza maagizo yake ya kuhakikisha kila mwananchi aliyewahi kuibiwa na taasisi za utoaji mikopo, na ana ushahidi, aweze kurejeshewa fedha zake na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza kwa bashasha na kulengwalengwa na machozi Mzee Kanyinga Abdallah ameeleza haamini anachokiona "...niliamini kuwa sitazipata pesa zangu kwa sababu wakopeshaji hawa wana nguvu na wana mtandao mkubwa. Namshukuru sana DC wetu wa Tunduru na Kamanda wa TAKUKURU kwa msaada wao...Mungu atawalipia".

Mwezi Aprili 2020, Mtatiro alitoa maelekezo kwa taasisi za utoaji mikopo, kuachana na biashara ya kuwadhulumu wananchi kwenye wilaya yake, na aliielekeza TAKUKURU kuchukua hatua kali sana.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad