HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 18, 2020

MGOMBEA UDIWANI KATA YA IGUMBILO BONIFACE KILAVE APITA BILA KUPINGWA


 


Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu amemtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwaWaandishi wa habari wakimsikiliza Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu akimtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwa 



Na Fredy Mgunda,Iringa.

MSIMAMIZI wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu amemtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwa baada ya wagombea wa vyama vingine kujiondoa kugombea udiwani kwenye kata hiyo.

Akitangaza maamuzi hayo msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu, alisema kuwa wagombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Wilbert Kilave na mgombea wa chama cha ACT WAZALENDO, Mahamad Rassa walimwandikia barua za kujiondoa kwenye uchaguzi huo huku wakiwa wameambanisha na viapo vya tamko la kujitoa vilivyotolewa mbele ya hakimu mnamo tarehe 17/11/2020

Alisema kuwa barua hizo za kujiondoa zilizingatia kifungu cha 50 cha sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa (uchaguzi wa madiwani) Sura ya 292 ya mwaka 2015 na kanuni zake.

Njovu aliongeza kuwa mgombea huyo wa udiwani aliyepita bila kupigwa atakabidhiwa hati ya kuchaguliwa kuwa diwani ya kata hiyo ya Igumbilo tarehe 8/12/2020 siku ambayo uchaguzi ulitakiwa kufanyika.

Aidha Msimamizi huyo wa uchaguzi alitangaza kuwa jimbo la Iringa Mjini litakuwa na madiwani wa chama kimoja ambacho ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee

Uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika kutokana na kifo kilichotokea cha tarehe 16/10/2020  na kumpa mamlaka ya kuitisha uchaguzi upya kwa mujibu wa kanuni ya 33(1) na (2) ya kanuni ya uchaguzi wa uchuguzi wa serikali za mitaa (uchaguzi wa madiwani),sura ya 292 ambazo zilipelekea msimamizi wa uchaguzi  wa jimbo la Iringa Mjini kutoa taarifa tume ya taifa uchaguzi kuhusu kifo cha mgombea udiwani wa chama cha mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad