Afisa
Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo
ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC)
kimetoa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari
Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo kuzielewa sheria zinazoongoza Tasnia
ya Habari nchini.
Mafunzo
hayo ya siku mbili ambayo yameanza leo Jumapili Novemba 15,2020 Mjini
Shinyanga yamekutanisha pamoja waandishi wa habari 23 kutoka mikoa ya
Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Mara.
Akizungumza
wakati akifungua mafunzo hayo, Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata
Ntwale amesema mafunzo hayo yatawawezesha waandishi wa habari kuzijua
sheria zinazohusu tasnia ya habari ili waweze kutekeleza majukumu yao
vizuri.
“Mafunzo
haya yanahusu haki za binadamu, Uhuru wa Kushiriki 'Civic Space' ambapo
tunawajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sheria mbalimbali
zinazogusa Tasnia ya Habari kama vile Kanuni za Mawasiliano ya
Kielekroniki na Posta 'Maudhui ya Habari Mtandaoni) 2020, Sheria ya
makosa ya mtandao 2015, Sheria ya Huduma ya Habari 2016 na Sheria ya
kupata habari 2016",amesema Ntwale.
Amesema
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu
sheria hizo ili waweze kufanya kazi katika mazingira salama na kwa
kujiamini ili kupunguza kesi zinazowakumba waandishi wa habari
zinazotokana na kukiuka sheria bila kujua.
"LHRC
inaendesha mafunzo juu ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa waandishi wa
habari nchini Tanzania katika Kanda saba na kwa Sasa imefikia Kanda ya
Ziwa ambapo tumeamua yafanyike mkoani Shinyanga",ameongeza Ntwale.
Afisa
Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo
ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa leo
Jumapili Novemba 15,2020 katika Ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini
Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa
Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo
ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Afisa
Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo
ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Washiriki wakiwa ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Waandishi wa habari/washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment