HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 3, 2020

Ni wiki ya kukata na shoka kwenye ulimwengu wa soka barani Ulaya

 *Mpira katika ubora wake! Tabiri na Ushinde!

UNADHANI itakuwa ni wiki ya namna gani kama haitokuwa na mechi za kukata na shoka na upinzani wa hali ya juu wa timu bora barani Ulaya? Wikiendi hii itakuwa ya aina yake ikipambwa na mechi mbalimbali za kibabe!

Kama unavyojua, moja ya ligi kubwa Ulaya – Serie A imeanza hivi karibuni. Wiki 2 zimeshapita na sasa ni muda ya kupata ladha ya wababe wa Ligi ya Italia.


Lazio watawakaribisha Inter Millan majira ya saa 10 jioni, Juventus na Napoli watachuana mjini Turin majira ya saa saa 3:45 usiku.


Msimu uliopita, Lazio ilikuwa ni kati ya timu zilizokuwa na nafasi ya kubeba kombe la Serie A – Scudetto. Kwa mara ya kwanza timu hii ilitishia utawala wa Juventus. Japokuwa, kuelekea michezo ya mwisho, Inter waliwapiku Lazio kwenye msimamo wa ligi na kumaliza nafasi ya 2 huku Lazio wakimaliza nafasi ya 4.


Juventus ndio mabingwa watetezi wa Serie A. Msimu uliopita, “bibi kizee wa Turin” alibeba kombe la 9 mfululizo na 36 kwa jumla. Baada ya kutolewa kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, Mauricio Sarri alifukuzwa kazi na Andrea Pirlo akachukua nafasi yake.


Mchezaji wa zamani na sasa kocha wa Juventus, atakutana na mchezaji mwenzake wa zamani kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Italia na AC MilanGennaro Gattuso.


Tuhamie kidogo La Liga, mchezo mkubwa ni kati ya Barcelona na Sevilla. Mtanange huu utachezwa saa 4 usiku. 

Timu hizi zinahistoria ya kuwa wapinzani wa muda mrefu. Wameshakutana mara 63 na Barca ameshinda mara 39 wakati Sevilla ameibuka mshindi mara 12 na wametoka sare mara 12 vilevile.


Ukweli ni kwamba, Sevilla hajawahi kumfunga Barcelona tangu mwaka 2015. Katika mechi 9 za mwisho, Barcelona ameshinda 7 na wametoka sare mara 2. Kwa takwimu hizi, haishangazi kuona Barcelona wanapewa nafasi ya kushinda licha ya Sevilla kuwa na kikosi bora zaidi.


Tutupie jicho kwenye Premier League, Manchester United na Tottenham watakutana saa 12:30 jioni. Huu ni mchezo wa muhimu kwa timu zote baada ya kumaliza michezo yao iliyopita kwa namna ya kushangaza ulimwengu.

Tukukumbushe tu, Tottenham walipoteza pointi 2 dhidi ya Newcastle kwa mkwaju wa penati dakika ya 97. Manchester United walipata ushindi dhidi ya Brighton Albion kwa mkwaju wa penati dakika ya 95, katika mchezo huo Brighton wangeweza kushinda goli 5 zaidi kutokana na kugonga mwamba mara 5.


Kimsingi, mpira upo katika ubora wake. Ni muhimu kujua ofa na odds kubwa zinakusubiri kupitia Meridianbet. Bofya hapa kujichagulia ukipendacho.

20 comments:

Post Bottom Ad