Dar
es Salaam. Bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter Hassan
Mwakinyo atautetea mkanda wake wa Chama cha WBF Novemba 13 dhidi ya
bondia wa Argentina Jose Carlos Paz.
Pambano hayo yamepewa jina la Dar Fight Night yameandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.
Mbali
ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito
huo huo wa Chama cha IBA. Pambano hilo limepangwa kufanyika kwenye
ukumbj wa Next Door Arena.
Mkurugenzi
wa The Jackson Group Sports Kelvin Twissa amesema siku hiyo mabondia
kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz, akiwamo
aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya.
Twisa alisema kuwa Zarika atazichapa na Patience Mastara wa Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.
Pia siku hiyo, bondia Abdallah Pazi maarufu kwa jina la Dullah Mbabe atacheza na Alex Kabangu wa DR Congo.
Alisema
kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua
vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri
katika mapambano yake.
"Siku
hiyo kutakuwa na pambano makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita,
Argentina, DR Congo, Kenya, Uganda, Zimbabwe na wenyeji Tanzania
watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za kulipwa wataona kitu
tofauti kabisa katika mchezo huo, " alisema Twisa.
Alisema
kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV na Asas ina uzoefu mkubwa
katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi
kufanya jambo la kihistoria hapa nchini.
"Tunataka
kuona mabondia wanaendelea kwa kupata mapambano mengi ya ngumi na
kinacho endana na kazi yao, tulifanya kazi na Mwakinyo kwa miaka mitatu
na kuona ufanisi wake, tumeamua kuendelea naye na mabondia wengine wa
Tanzania, tutaubadili mchezo wa ngumi nchini," alisema.
Kwa upande wake, Mwakinyo alisema kuwa hiyo ni fursa kwake na kuahidi kufanya vyema siku hiyo.
"Namshukuru
Twisa na kampuni ya Jackson Group Sports ambao wameonyesha nia ya
kuubadili mchezo wa ngumi za kulipwa, sitawaangusha watanzania," alisema
Mwakinyo.
Mwakilishi
wa WBF nchini Tanzania, Chatta Michael alisema kuwa rais wa shirikisho
hilo, Goldberg Howard atasimamia mapambano hayo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twisa (wa pili kulia)
akiutambulisha mkanda wa mabara wa WBF ambao bondia Hassan Mwakinyo (wa
pili kulia) atautetea dhidi ya bondia Jose Carlos Paz Novemba 13 kwenye
ukumbi wa Next Door Arena, Masaki. Wa kwanza kulia ni bonda Dulla Mbabe
na wa kwanza kushoto ni bondia Zulfa Macho
Mkurugenzi
wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twisa (katikati) akizungumza
wakati wa utambulisho wa mapambano ya Dar Fight Night yaliyopangwa
kufanyika Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door Arena kati ya bondia
Hassan Mwakinyo (wa pili kulia) dhidi ya bondia Jose Carlos Paz wa
Argentina. Wa kwanza kulia ni bonda Dulla Mbabe na wa kwanza kushoto ni
bondia Zulfa Macho na pili kushoto ni mwakilishi wa WBF Tanzania, Chatta
Michael.
No comments:
Post a Comment