HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 1, 2020

DKT. MAGUFULI APIGA SIMU KUWAOMBA KURA WANA-USHETU

 

 

Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa eneo la Runzewe, Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe, katika mkutano wa kampeni, Oktoba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko, azungumza mbele ya Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, eneo la Runzewe, Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe, katika mkutano wa kampeni, Oktoba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amepiga simu na kuwaomba wakazi wa Ushetu wampigie kura za kutosha ili awatumikie.  


Ameongea nao leo jioni (Alhamisi, Oktoba mosi, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa Ushetu kupitia simu aliyompigia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamilangano, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.


“Watu wa Ushetu ninawashukuru sana kwa kumpitisha bila kupingwa Engineer Kuandikwa. Mimi niko Tunduma, nilitamani niwe hapo na ninyi lakini nimemtuma Waziri Mkuu aje kuniombea kura. Yote ambayo atazungumza Majaliwa nimemtuma mimi, nawatakia mkutano mwema,” amesema.

 

Alisema ahadi yake aliyoitoa ya kutengeneza barabara ya Ushetu-Kahama iko palepale na kwamba akimaliza uchaguzi atafika kuwatembelea. “Naikumbuka hiyo barabara ya Ushetu kwenda Kahama, tutaitengeneza kwa kiwango cha lami. Naomba kura zenu pamoja na madiwani wote wa CCM.”


Baada ya Rais Dk. Magufuli kuzungumza na wananchi, Mheshimiwa Majaliwa aliwataka wakazi hao wamchague kwa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa urais, wabunge na madiwani wa CCM.

Kwa upande wake, Eng. Kwandikwa alisema wananchi wa Ushetu wamepata mafanikio chini ya Rais Dk. Magufuli akitoa mfano wa ujenzi wa barabara za wilaya zilizojengwa kwa kiwango cha lami kilomita 1200 kutoka kilomita 400 mwaka 2015.

Pia alisema serikali ya awamu ya tano imeweka umeme katika vijiji 58 kati ya 112 na vilivyobaki vitapatiwa umeme. Kuhusu elimu, Eng. Kwandikwa alisema wamepokea sh. bilioni tano kwa shule za msingi, sekondari na miradi ya maji inaendelea katika wilaya hiyo.

 

Eng. Kwandikwa aliwataka wananchi wa Ushetu wamchague Rais Dk. Magufuli ili awaletee maendeleo katika nyanja mbalimbali zikiwemo huduma za afya, umeme, maji na barabara

 

Mheshimiwa Majaliwa ambaye amemaliza ziara yake ya siku moja mkoani Geita yuko Mkoa wa Shinyanga akiendelea kutafuta kura katika wilaya mbalimbali.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad