Na Jusline Marco;Arumeru
MKUU
wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mekabidhi hundi ya shilingi millioni
165 kwa vikundi 37 ikiwa ni awamu nyingine ya kwanza ya mikopo
iliyoanza kutolewa ambayo inawalenga wanawake, vijana na walemavu.
Akikabidhi
hundi hiyo Muro amesema hadi sasa zaidi ya vikundi 550 vya wananchi
wilayani humo tayari vimepatiwa mikopo kupitia fedha zinazotokana na
asilimia 10 ya Mapato ta ndani ya Halmashauri ambapo jumla ya shilingi
bilioni 3 zimeishatolewa katika vikundi mbalimbali vilivyoundwa na
makundi hayo ya wananchi Ili kuwakwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa
katika kipindi cha miaka mitano Halmashauri zote mbili za Meru na Arusha
vijijjni zimeweza kufikia malengo kwa kuyafikia makundi yote matatu kwa
haraka kutokana na mwitikio wa wananchi wa kujitokeza na kuanzisha
miradi ambayo imekuwa endelevu hali iliyopelekea kuwa na wanufaika 6000
waliopatiwa mikopo hiyo kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka kufika mwezi
September 2020/202.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa
utoaji wa mikopo isiyokuwa na riba kupitia asilimia 10 ya makusanyo ya
fedha za ndani za Halmashauri, mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii wa
Halmashauri ta Arusha vijijini Bi. Angelah Mvaa amesema Halmashauri
hiyo inaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuanzisha na
kuwajengea uwezo kupitia program ya mafunzo maalum kwa vikundi wanufaika
itakayowasaidia kuweza kuzitumia fedha hizo katika njia iliyokusudiwa.
Wakizungumza
mara baada ya kukabidhiwa hundi hiyo baadhi ya wanawake na vijana mbali
na kumpongeza, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika kusimamia
alichoahidi katika ilani ya Uchaguzi katika kipindi cha mwaka 2015/2020
wamesema kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kuwafikia na
kuyabadilisha maisha yao imefanikiwa kwa kiasi likubwa.Aidha
serikali imeendelea kuwajali na wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
kwa kuhakikisha hawaachwi nyuma kwenye uchumi wa kati ambapo mmoja kati
ya wanufaika wa mikopo hiyo, Bi.Suzan Eliamsuri kutoka kata ya Mateves,
amesema mikopo hiyo imekuwa mkombozi wao.
Hata hivyo hafla ya
makabidhiano ya fedha hizo imekwenda sambamba na utoaji wa mafunzo ya
ujasiriamali kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu sambamba na
uanzishwaji wa vikundi vingine ambavyo vitaendelea kujengewa uwezo kabla
ya kukabidhi fedha zingine katika awamu ijayo.
No comments:
Post a Comment