Charles James, Michuzi TV
CHUO
cha Uhasibu Arusha (The Instistute of Accontancy Arusha IAA) ambacho
kipo chini ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kinatarajia
kufungua tawi (Campas) la Chuo hicho katika Mkoa wa Dodoma lengo likiwa
kuunga Mkoano Jitihada za Serikali katika Sekta ya Elimu .
Akizungumza
leo na wandishi wa habari jijini Dodoma Mkuu wa Chuo hicho Profesa
Eliamini Sedokeya amesema ili kuweza kuendana na jitihada za serikali
wameona ni vyema kama chuo wakatoa mchango wao katika kuhakikisha kwamba
wanaongeza tawi (Campas).
‘’ Kuzingatia kuwa nchi imehamia
katika Makao Makuu ya nchi yamehamia Dodoma kwahiyo sisi kama chuo
tukasema na sisi ni wajibu na niwakati muafaka wa sisi kwenda Dodoma ‘’
Amesema
toka awamu ya tano ilivyoingia madarakani kumekuwa na mabadiliko
makubwa katika sekta ya Elimu kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Jonh Pombe Magfuli alikuja na mpango wa kutoa Elimu bure
kwamaana ya Elimu bila malipo katika ngazi za msingi na sekondari hivyo
hiyo imepelekea mahitaji katika vyuo kuongezeka sana
‘’ kwahiyo
unaona ongezeko hilo wote labda hawataweza kwenda high school lakini
vile vile wakija vyuoni masalani inawezekana tusiweze kuwapokea wote
kwahiyo ili kuendana na jitihada za serikali tukaona kama chuo tutoe
mchango wetu kuhakikisha kwamba tunakua.’’
Profesa Sedoyeke
amesema mpaka sasa wametafuta katika la eneo Njendengwa wamelilipia
ambapo kwa sasa wapo katika hatua za mwisho kwaajili ya kupata hati na
tayari michoro na taratibu nyingine za ndani za kibali kwaajili ya
kuanza kujenga zimekwisha kuanza.
‘’ Kwa hiyo sasahivi kufungua
tawi (Campas) Dodoma ni kitu ambacho kipo tayari kwenye mwendo na
tunategemea mwakani tukawa na tawi (Campas) ambayo iko kamili inayotoa
kozi zote kuanzia ngazi ya cheti mpaka Masters’’ Amesema Prof Sedoyeke.
Amesema
mpaka sasa wanakozi hamsini (50) huku wakijiendesha katika Matawi
makubwa matatu ikiwemo Arusha,Babati na Dar es salaam.
‘’mpaka
sasa tunawanafunzi takribani elfu tano tukiwa na waajiriwa kama mia
mbili ishirini vile vile chuo kimeendelea kushirikiana na taasisi
mbalimali kama jeshi ,"
Chuo cha uhasibu Arusha ni chuo cha
Serikali kilicho anzishwa miaka ya themanini kama kituo cha kutengeneza
wataalamu wa uhasibu baada ya hapo serikali iliona umuhimu wa kuwa chuo
kamili ,sheria ya Namba moja (1) 1990 ikaanzisha chuo rasmi ambapo kwa
sasa wanakwenda miaka thelathini ya chuo hicho .
Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha IAA akifafanua jambo kwa wandishi wa habari
jijini Dodoma alipokua akitangaza azma ya Chuo hicho kufungua tawi lake
jijini Dodoma ukiwa ni mpango wao wa kuunga mkono juhudi za serikali
kuhamia Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment