HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 10, 2020

“CHANGAMKIENI FURSA ZA MWENDOKASI NA RELI YA KISASA”, ASEMA MHANDISI EVARIST NDIKILO

Wakulima wa mpunga na mboga mboga wa bonde la umwagiliaji la Ruvu wilayani Bagamoyo wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za usafiri zitakazoambatana na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ikiwemo reli ya kisasa inayopita wilayani humo na usafiri wa mwendokasi kati ya Pwani na Dar es Salaam.

Akizungumza katika kilele cha siku ya wanachama wa kilimo cha umwagiliaji wa Ruvu (CHAURU) Jumamosi  ya tarehe 10 mwezi huu, Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo amewahimiza wakulima hao kuhakikisha kuwa hawafanyi mchezo na fursa hiyo. Amesema usafiri ndiyo kichocheo kikubwa cha kukua kwa bishara baina ya maeneo tofauti. 

Mhandisi Ndikilo amesema kuwa kukamilika kwa barabara ya mwendokasi katika ya Pwani na Dar es Salaam ni uhakika kuwa mazao ya wakulima na hasa yale ya mboga mboga na matunda hayatatumia zaidi ya dakika 45 kufika Dar es salaam. Hiyo ni kusema kuwa bidhaa hizo zitafika sokoni zikiwa na ubora wake ule ule na hivyo mkulima kupata bei bora. Vivyo hivyo na usafiri wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Mhandisi Ndikilo amesema itakuwa rahisi kusafirisha mazao kati ya Pwani na mikoa ya jirani ikiwemo Mji Mkuu Dodoma, ambao utakuwa masaa machache tu kutoka hapa.

Amewahimiza kuzingatia ubora na kuongeza kuwa mkoa uko tayari kuwajengea wakulima hao chumba baridi (cold room) kwa ajili ya uhifadhi wa mazao ya mboga mboga na matunda.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa ameshazungumza na Benki ya Kilimo Tanzania ili kuona umuhimu wa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima hao, na kutaarifu kuwa Benki hiyo tayari ina andiko la CHAURU na wanalifanyia kazi.



Baadhi ya mashamba ya mpunga yaliyopo katika eneo la CHAURU
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, viongozi wa CHAURU, pamoja na wadau wa kilimo wakishuhudia uvunaji wa mpunga katika moja ya shamba lililopo kwenye eneo la CHAURU wakati wa maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU).
Uvunaji wa mpunga ukiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Meneja Shamba wa CHAURU James Hangi alipokuwa anatoa maelezo kuhusu maji wanayoyatumia kwenye kilimo katika shamba la CHAURU.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua shamba la nanasi lililopokatika eneo la shamba la CHAURU wakati wa kutembelea shamba hilo na kujionea shughuri zinazofanyika katika eneo hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU).
Meneja Ufundi wa Agricom Africa Ltd,  Philipo William akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu kampuni hiyo inavyowakopesha na kutoa mikopo ya vifaa vya kilimo vya kisasa kwa wakulima ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) itakayoendana na maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua baadhi ya bidhaa za Agricom Africa Ltd alipokuwa anatembelea mabanda ya wakulima pamoja na wadau wa kilimo wakati wa wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiangalia moja na bidhaa inayotumika kurutubisha ardhi alipokuwa  anatembelea mabanda ya wakulima pamoja na wadau wa kilimo wakati wa wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020
Mwenyekiti wa The winners group,  Winjuka Mashenene akifafanua kuhusu namna walivyojipanga kama vijana kuwekeza kwenye kilimo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa anatembelea baadhi ya mabanda mbalimbali wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa apokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu mbegu mbalimbali za mpunga zinazoweza kuinua kilimo na namna ya mkulima kuzitumia mbegu hizo wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Meneja wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Victoria Olotu  akitolea ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu mchele  pamoja na Korosho zinazolimwa katika  hilo alipokuwa anatembelea baadhi ya mabanda mbalimbali kwenye maonesho yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba, 2020.
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha kizungumza kuhusu historia ya ushirika huo ulioanzishwa mwaka 2002 pamoja na changamoto wanazozipata ndani na nje ya ushirika huo wakati wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake kwa viongozi na Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) waliofika kumsikiliza wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.

Baadhi ya Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa zawadi kwa wadau mbalimbali wa kilimo wa wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  tuzo ya shukrani kutoka kwa uongozi wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akionesha tuzo ya shukrani aliyopewa na uongozi wa CHAURU kwa kuweza kuwahamasiha kulia kilimo cha kisasa ili kufikia malengo waliyojiwekea kama ushirika wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wakulima wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo tarehe Oktoba 10, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa kwenye picha za pamoja na viongozi, wanachama na wadau wa kilimo wakati wa kufunga maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad