Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
 katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi wa Mbio za  NMB 
Marathon  baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao kwenye viwanja vya 
Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Wa nne kulia ni 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki , wa 
tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili 
kulia   ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna  na kulia 
ni Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Profesa Lawrence 
Maseru. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa,
 Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi 
ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.

Waziri Mkuu, Kassim 
Majaliwa  akisalimiana na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri 
Mkuu,  Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati alipowasili kwenye  viwanja 
vya Mlimani City jijini Dar es salaam kufungua Mbio za NMB Marathon  na 
kutoa zawadi kwa washindi Septemba 12, 2020.  Wa pili kulia ni Mkuu wa 
Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi 
ya Wakurugenzi ya NMB,  Dkt. Edwin Mhede.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
 Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati 
alipohitimisha  Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City 
jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi 
ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa 
Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji 
Mkuu wa Kampuni ya Sanlam  East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto
 ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha 
hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye 
ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


No comments:
Post a Comment