HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 2, 2020

WANAWAKE WATAKIWA KUTUMIA WASAIDIZI WA KISHERIA KUPATA HAKI ZAO


NA HAMIDA RAMADHANI-CPC DODOMA.

JAMII imetakiwa kuacha uoga na badala yake imeaswa kuwatumia wasaidizi wa msaada wa kisheria hasa wanawake pale wanapo kandamizwa kwenye suala zima la haki zao za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana,Afisa Ufuatiliaji Tathimini Hamisa Hamad kutoka Pemba kwenye kikao cha tathimini amesema lengo la kikao ni kufanya mapitio ya mambo ambayo tumeyatelekeza ndani ya mwaka.

Katika kikaokazi hiki tunatekeleza mapitio tuliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja na Kama inavyojulikana kwa sisi upande wa Zanzibar msaada wa kisheria ulikua mgeni kwetu kutokana na mila na desturi na dini.Hamisa Hamad 

Amesema Msaada wa kisheria kwa Zanzibar ilikua ni kitu kigeni kutokana na mila na desturi na dini lakini baada ya kufika mwaka 2007 baada ya shirika la Legal services facility LSF)kufika ndipo wanawake 850 waliamka na kuanza kutoa taarifa za kikatili wanazo fanyiwa na wenza wao na kupatiwa msaada wa kisheria.

"Zamani kwa sisi Awaafrika kwa mila zetu na deaturi ilikua ni ngumu kutoka kwenda kumshitaki mwenza wao eti tu kwakukosea au kwakufanyia tendo la ukatili hali iliopelekea sisi wasaidizi wa kisheria kukosa takwimu sahihi za kuwatambua ni wanawake wangapi waliofanyiwa ukatili wa kijinsia"amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa

Aidha amesema katika mila za kiafrika wanawake na watoto ndio wanaongoza kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

MAFANIKIO.

Amesema baada ya kuja kwa wasaidizi wa msaada wa kisheria wanawake wengi wamejitokeza na kuanza kudai haki zao za msingi ikiwemo kudai ardhi ,asilimia 99 ya wanzanzibar ni waislam.

Amesema katika dini ya kiislam imeainisha wazi mwanamke akifa anatakaiwa apewe haki zake kadhaa na mwanaume haki kadhaa lakini jambo hilo limekuwa likikiukwa na wanaume wamekua wakiwakandamiza.

"Sasa ni vyema wanawake wote kujitokeza katika kudai haki zao kwani mwanamke ana haki zake ya kutunzwa kupewa mirathi na ikitokea umeachwa dai haki zako na kama ikitokea hata mwaume amefariki mwanamke anatakiwa apewe haki zakezote "amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa

Naye Afisa Ufuatiliaji na Tathimini kutoka mkoani Lindi Nelson Choaji amesema kazi yao kubwa katika mkoa wa lindi ni kuhakikisha upatikanaji wa haki katika mkoa wa Lindi unapatikana.

Hata hivyo amesema kwa upande wa Lindi Legal Service Facility imekua ikiwapa nguvu wasaidizi wa kisheria kuhakikisha wanawafikia watu wote wenye changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika jamii.

Tatizo kubwa la mikoa ya pwani kesi nyingi tunazokumbana nazo ni za wanaume kutekeleza familia zao mi nitoe wito tu kwa kina mama kuwatafuta wasaidizi wa msaada wa kisheria pindi wanapo hitaji haki zao za msingi. Nelson Choaji

Legal Service Facility ni Shirika lisilo la kiserikali lenye makao Makao Makuu yake jijini Dar es salaam lengo kuu la uanzishwaji wake ni kusaidia jamii kupata haki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),(pichani kati) Lulu Ng'wanakilala, akifafanua jambo mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jana jijini Dodoma.Picha na Michuzi JR.
Washiriki mbalimbali wa kikao hicho wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na baadhai ya Wajumbe wa kikao hicho ndani ya jiji la Dodoma 
Meneja Mawasiliano wa LSF, Jane Matinde akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa katika kikao kazi hicho kilichofanyika ndani ya jiji la Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad