HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 29, 2020

WANAJAMII 2,667 WANUFAIKA NA ELIMU Y KUPINGA UNANYASAJI

 

Afisa Tathimini na ufuatiliaji wa TAMWA Zanzibar, Mohamed Khatib Mohamed akizungumza na wanamtandao huo. Seif  Sharif Makame, miongoni mwa wanamtandao huo akichangia mada wakati wa kikao hicho.
anamtandao wakishiriki kikao cha kupokea na kujsdili ripoti ya
utekelezaji wa majukumu yao.

Asha Juma Omar, ambae ni mwanamtandao wa kupinga udhalilishaji akiwasilisha ripoti ya ufuatiliaji na utoaji wa elimu katika jamii.

Na Gaspary Charles, TAMWA PEMBA
MTANDAO wa kupinga udhalilishaji Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba umefanikiwa kutoa elimu kwa wanajamii 2,667 kwa Mwezi wa Agosti na Septemba, ambapo watu 1,452 sawa na asilimia 54 kati yao wakiwa ni
wanawake na wanaume 1,215 sawa na asilimia  46 ya wote waliofikiwa katika kipindi hicho.

Hayo yamebainishwa na wanamtandao huo wakati wa kikao cha kujadili
maendeleo ya kazi za kutoa elimu, kufuatilia na kuibua kesi hizo
kilichofanyika katika Ofisi za TAMWA Pemba.

Seif Sharif Makame miongoni mwa wanamtandao huo alisema katika kipindi
hicho pia wamefanikiwa kuibua na kufuatilia kesi Nane ambapo kati ya
kesi hizo Nne zinahusiana na matukio ya ubakaji.

“Katika juhudi za kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii
tulifanikiwa kuibua kesi Nane huku kesi Nne zote zikiwa ni kesi za
ubakaji,” alisema.

Kwa upande wake Asha Juma Omar, alisema wazazi wanatakiwa kuwajibika
ipasavyo kwa kuwafuatilia watoto wao  kwani  kufanya hivyo itasaidia
kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

Alisema kupitia utoaji wa elimu na ufuatiliaji wa kesi hizo katika jamii
wamebaini kuwepo kwa mashirikiano madogo katika kuripoti matukio ya
ushalilishaji jambo linalopelekea kuongezeka kwa viutendo hivyo katika
jamii.

Katika hatua nyingine alibainisha kuwa uwepo wa mikutano ya kampeni
umeathiri kwa kiasi kikubwa jihudi za ufikiaji wa jamii nyingi kutokana
na wengi wao kushindwa kuhudhuria katika mikutano yao.

“Mikutano ya kampeni imekuwa ni changamoto kubwa  kwetu katika harakati
hizi za ufikishaji wa elimu kwa jamii kwani sehemu nyingi tulizokuwa
tunatembelea  wengi wao sasa wanajikita zaidi katika mikutano ya
kisiasa,” aliongeza.

Mapema akizungumza katika kikao hicho, Afisa Tathimini na ufuatiliaji wa
TAMWA Zanzibar, Mohamed Khatib Mohamed aliwasisitiza wanamtandao hao
kuendelea kuzifuatilia kwa ukaribu kesi zilizoibuliwa ili kuhakikisha
wanawasaidia wahanga wa matukio hayo kupata haki zao katika vyombo
husika.

Alisema, “lengo na jukumu la uwepo wa mitandao ya kupinga udhalilishaji
katika jamii sio tu kuibua kesi na matukio hayo bali ni kuhakikisha
tunaziibua na kuzifuatilia kuanzia hatua ya mwanzo hadi mwisho.

Nae Mratibu wa TAMWA ofisi ya Pemba, Fat-hiya Mussa Said aliwataka
wanamtandao huo kuongeza kuvu zaidi za kufuatilia kesi ambazo tayari
zimeibuliwa ili ziweze kufikishwa katika ngazi husika za kisheria.
Aidha aliiomba jamii kuendelea kutoa mashirikiano kwa wanamtandao huo na
kuacha tabia za kuficha matukio ya udhalilishaji ili wahusika wa vitendo
hivyo waweze kuchukuliwa hatua kisheria.

Kikao hicho ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa kuongeza nguvu
kwenye juhudi za mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar
unaotekelezwa na Chama cha Waandishi wa Habari -TAMWA Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad