HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 15, 2020

SIRRO - WANANCHI TUSIWACHAGUE WASIOKUWA WATANZANIA

 

Na Abdullatif Yunus MichuziTv.

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Kamanda Saimon Sirro amewataka Wananchi hususani Watanzania kuwachagua Viongozi Watanzania kwa Utaifa wao, na kinyume na hapo watakuwa wanafanya kosa kubwa la kuliingiza Taifa matatani.

Kamanda Sirro ameyasema hayo akiwa Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, alipofika Eneo la Tukio kujionea maafa yaliyosababishwa na Moto na kupelekea Bweni la Shule ya Msingi Byamungu kuteketea, huku Watoto 10 wakipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Kamanda Sirro amesema kuwa kumpa Uongozi asiyekuwa Raia Ni kufanya kosa kubwa, kwani muda wowote anaweza kuondoka, na kuwasihi Wananchi wanawachagua Watanzania.

Aidha Sirro amesema kwa upande wa Jeshi la Polisi wapo Tayari kushughulika na wachache ambao wamezoea vurugu, na kwamba watakaojaribu kufanya vitendo hivyo Vya Uvunjifu wa Amani watakuwa nao bega kwa bega, na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi litatenda haki kwa Vyama Vyote Vya Siasa pasipo kubagua kuanzia kwenye Mikutano yao Hadi siku ya kupiga Kura.

Wilaya ya Kyerwa Ni kati ya Wilaya inayopakana na Nchi za Rwanda na Uganda hivyo kumekuwa na vitendo Vya Wenyeji (Watanzania) kuwakaribisha Raia kutoka Nchi jirani na kuishi nao bila vibali Maalum na mwisho wa siku kupelekea Raia hao kuishi Nchini na kushiriki shughuli nyingine zikiwemo za Kisiasa, duru zikieleza wapo ambao waliwahi kupewa Uongozi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad