HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 28, 2020

SIMANZI NA VILIO VYATAWALA MAZISHI MWENYEKITI WA SENET MKOA WA IRINGA EMMANUEL MLELWA.

 

Na Shukrani kawogo, Njombe

Simanzi na vilio vimetawala kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi katika kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho  Mwenyekiti wa Senet mkoa wa Iringa Emmanuel Polycup Mlelwa  kijiji kwao Ruhuyo wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama hicho, viongozi wa kidini pamoja na viongozi wa serikali ambao kwa pamoja wamelaani vikali kitendo hicho cha mauaji.

Akizungumza katika mazishi hayo mkuu wa mkoa wa Njombe Injinia Marwa Rubilya amesema atahakikisha wale wote waliohusika na kitendo hicho Cha mauaji anachukuliwa hatua Kali ya kisheria.

Aidha kwa upande wa mmoja wa ndugu wa marehemu Silvanus Msigwa amesema mnamo September 20 mwaka huu walikuwa wanamtafuta ndugu yao kwenye simu lakini walikuwa hawampati wakati si kawaida yake ndipo wakatoa taarifa polisi ili kuweza kupata msaada.

Aliongeza kuwa September 26 mwaka huu walipokea taarifa kutoka hospital ya Kibena ikiwajulisha uwepo wa mwili wa mtu ambaye ndugu zake hawajapatikana na walipoenda ndipo walipomtambua kuwa ndiye ndugu yao.

Frank Awasi ni mjumbe wa halmashauri kuu Taifa ambaye alifika msibani hapo akimuwakilisha Rais John Pombe Magufuli ambapo ametoa fedha ya rambirambi kiasi Cha sh. milioni tano huku viongozi wengine wa ccm mkoa, wilaya, wabunge, pamoja na wanafunzi wa chuo alichokuwa anasoma wakiwasilisha rambi rambai zao.
Vijana mbalimbali wakishusha jeneza kaburini lililobeba mwili wa marehemu Emanuel Polycup Mlelwa.
Mbunge mteule wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akitoka kutoa sadaka katika ibada ya mazishi ya Mwenyekiti wa Senet mkoa wa Iringa Emmanuel Polycup Mlelwa iliyofanyika katika kanisa la KKKT lililopo kijijini kwao Ruhuyo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Injinia Marwa Rubilya,,(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza na wananchi walipokuwa makaburini
Vijana wa green Cards wakiwa wamebeba sanduku lililobeba mwili wa Emmanuel Polycup Mlelwa.
Viongozi wa dini wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuesa Mwenyekiti wa Senet mkoa wa Iringa Emmanuel Polycup Mlelwa
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi ya Emmanuel Polycup Mlelwa wakiwa wameshika maua kwaajili ya kuweka kwenye kaburi. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Stainley Kolimba, Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa Frank Awasi, Mwenyekiti wa CCM mkoa Jasel Mwamala
Mbunge mteule wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Emanuel Polycup Mlelwa.
Kaburi alilolazwa Mwenyekiti wa Senet mkoa wa Iringa Emmanuel Polycup Mlelwa.
Mbunge mteule jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (katikati) akiwa ameshikana mikono na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Njombe.
Msemaji wa familia Silvanus Msigwa (aliyeshika kipaza sauti) skitoa wasifu wa marehemu
Mwili wa marehemu Emanuel Polycup Mlelwa ukiwa nyumbani kwao katika kata ya Madope iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume akitoa hesma za mwisho kwa marehemu Emanuel Polycup Mlelwa.


Muwakikishi wa Rais John Pombe Magufuli ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu Ccm Taifa, Frank Awasi akikabidhi fedha za rambirambi kiongozi wa dini kiasi Cha shilingi milioni tano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad