HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 4, 2020

SERIKALI YAZINDUA KADI ZA KIELEKTRONIKI KWA AJILI YA UWANJA WA MKAPA

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi amezindua matumizi ya awali ya kadi za kielektroniki zitakazotumika kuingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kadi hizo zitatumika katika matukio mbalimbali ya kimichezo ndani ya Uwanja huo.

Mfumo huo mpya wa kadi ulianza kutumika katika siku ya Simba (Simba Day) na baadae kilele cha Wiki ya mwananchi.

Kadi hizo zitatumika pia kwa matumizi mengine tofauti na kuingua Uwanjani pale mhusika atakapokuwa ameweka salio kwenye kadi hiyo.

Kwa matumizi ya kadi hiyo, kila kadi moja itatumika kununua tiketi moja na itasajiliwa kwa namba ya mtu mmoja tu.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua kadi za Kielektroniki zitakazotumika kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt Hassan Abbas akikata utepe kuashiria kuanza kwa matumizi ya kadi za Kielektroniki zitakazotumika kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt Hassan Abbas akionesha mfano wa kuchanja  kadi baada ya kuzindua mfumo huo wa Kielektroniki  utakaotumika na mashabiki kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt Hassan Abbas akionesha kadi yake  baada ya kuzindua kadi za Kielektroniki zitakazotumika kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad