SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA BILIONI 32.9 KUTOKA AIRTEL - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 2, 2020

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA BILIONI 32.9 KUTOKA AIRTEL

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akipokea Hundi ya Mfano ya shilingi bilioni 18.99, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel-Tanzania, Bw. Gabriel Malata, ambayo ni sehemu ya shilingi bilioni 32.9 ambazo Airtel imeilipa Serikali ikiwa ni gawio na michango ya maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Wanaoshuhudia kuanzia kulia ni Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbutuka, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Dkt. Zainabu Chaula na Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania, Bw. George Mathen (kushoto).

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akimpongeza Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka mara baada ya kupokea Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi bilioni 32.99 ni gawio la Tsh 18.9 bilioni pamoja na michango ya Tsh 14 bilioni kwa mwaka 2019/20 toka kwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Airtel Tanzania Bw, Gabriel Malata. Pamoja nao wakwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Dokta Zainabu Chaula, na Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania George Mathen (kushoto). Hafla hiyo imefanyika Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza wakati wa halfa ya kupokea gawio na michango kutoka Kampuni ya Airtel Tanzania, ambapo Serikali imepokea kiasi cha Sh. Bilioni 32.99 jijini Dodoma, zikiwemo shilingi bilioni 18.99 za gawio na shilingi bilioni 14 za michango ya maendeleo, Hafla ya makabidhiano imefanyika Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania, Bw. Gabriel Malata, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gawio na michango ya maendeleo kwa Serikali, Jijini Dodoma. Serikali inamiliki asilimia 49 ya hisa katika Kampuni hiyo na Kampuni ya Bharti Airtel inamiliki asilimia 51.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano akifafanua jambo baada ya Kampuni hiyo kutoa gawio na michango ya maendeleo kwa Serikali yenye thamani ya shilingi bilioni 32.99. Kuanzia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. George Mathen, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Airtel Bw. Gabriel Malata na wa tatu kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Benny Mwaipaja, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipamngo Bw. Doto James akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. George Mathen akifafanua jambo baada ya Kampuni yake kuipatia Serikali gawio na michango ya maendeleo ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 32.99 wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara hiyo baada ya Serikali kupokea gawio na michango ya maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 32.99 kutoka Kampuni ya Airtel Tanzania jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kampuni ya Airtel Tanzania, wakati wa hafla ya utoaji wa gawio na michango ya maendeleo kwa Serikali, ambapo Kampuni hiyo imetoa Shilingi bilioni 32.99, Jijini Dodoma.


Charles James, Michuzi TV


SERIKALI imepokea hundi ya gawio kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel la Sh Bilioni 32.9 ambapo Bilioni 18.9 ni gawio kwa serikali kwa mwaka huu na Bilioni 14 ikiwa ni mchango kwa serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.


Gawio hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, Gabriel Malata na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James leo jijini Dodoma.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Katibu Mkuu Dotto James amewashukuru na kuwapongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Airtel kwa kuhakikisha gawio linalipwa serikalini na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwetea watanzania maendeleo.


Dotto amezihimiza kampuni zingine ambazo serikali ina hisa hata kama ni asilimia moja kuhakikisha zinajiendesha kwa ufanisi na kulipa gawio stahiki serikalini.


" Nawapongeza sana Airtel kwa namna ambavyo mmejitoa katika kuiunga mkono serikali yetu na kuenda sawasawa na makubaliano yetu, gawio la Bilioni 32 limewafanya kuwa kampuni ya kwanza ambayo serikali ina hisa nayo kutoa gawio kubwa la namna hii.


Nitoe wito kwa mashirika ya umma na kampuni ambazo bado hazijatoa au zile zinazotoa gawio dogo zijitathimini na kuhakikisha zinafanya vizuri na kulipa gawio serikalini ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo," Amesema Dotto.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, Gabriel Malata amesema wao kama wabia wa serikali wataendelea kushirikiana katika kuwaletea maendeleo watanzania.


Amesema Airtel imeendelea kuchangia shughuli za maendeleo kwa kutoa kiasi cha Sh Bilioni 2.3 kusaidia ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambayo itaenda kuwa msaada mkubwa kwa watanzania.


" Tunajitahidi kuendelea kuwa mojawapo ya Kampuni zinazogusa maisha ya watanzania wenzetu, ndio maana tumetoa ajira rasmi 500, ajira mwambata 350,000 kupitia uuzaji wa vocha na huduma za kifedh.


Pia tumeingia makubaliano na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ambapo tumeanzisha programu inayoitwa V Somo inayowezesha wanafunzi kusoma bila kwenda darasani na mpaka sasa wanafunzi 17493 wameshajisajili," Amesema Malata.


Nae Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Zainab Chaula amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kwa ufanisi wake katika kusimamia urejeshaji wa gawio hizo huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano wa Airtel.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad