
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati
alipohitimisha Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City
jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha
hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye
ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi wa Mbio za NMB
Marathon baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao kwenye viwanja vya
Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Wa nne kulia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki , wa
tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili
kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence
Maseru. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa,
Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.

Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati alipowasili kwenye viwanja
vya Mlimani City jijini Dar es salaam kufungua Mbio za NMB Marathon na
kutoa zawadi kwa washindi Septemba 12, 2020. Wa pili kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.
No comments:
Post a Comment