Mapema leo Kamishna wa Operesheni
na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini,CP Liberatus Sabas(kushoto)
amewasili mkoani Morogoro kwaajili ya ukaguzi wa utayari kwa Askari
mkoani humo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani,(kulia) Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad
Mutafugwa (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP
Liberatus Sabas akikagua Paredi la kutuliza ghasia (riot drill )paredi
hilo limeundwa na askari Polisi kutoka Mkoa wa Morogoro wakati wa
mazoezi ya utayari kwaajili ya kukabiliana na uhalifu. (PICHA NA JESHI
LA POLISI)
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Liberatus Sabas
akizungumza na Maofisa na Askari Polisi wa vyeo mbalimbali mkoani
Morogoro baada ya kukakugua mazoezi ya utayari yaliyofanywa na askari wa
mkoani humo.CP Sabas amewataka Maofisa na askari hao kufanya kazi kwa
bidii na kwa weredi kwa lengo la kuhakikisha nchi inaendelea kuwa kisiwa
cha amani. (PICHA NA JESHI LA POLISI)
No comments:
Post a Comment