HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 30, 2020

WANUFAIKA TASAF WAPONGEZA MPANGO WA KUWANUSURU NA UMASKINI WAOMBA KUENDELEA KUSAIDIWA.

 Hawa Hamisi, kati kati na mume wake Said Kakwamba wakiwasikiliza wahariri na waandishi wa vyombo vya habari nchini (hawapo pochani) katika ziara ya mpango kazi baina ya wahariri na Watendaji wa TASAF.

 Edna .. mkazi wa  kijiji cha Mkambalani Morogoro akiwalezezea wahariri wa vyombo vya habari namna TASAF ilivyomsaidia mpaka amefanikiwa kununua mashine ya kutengeneza karanga, kiwanja, kusomesha watoto na mpaka sasa ameweza kujinyanyua kiuchumi wakati wa ziara ya kikao kazi  kazi kati yao na watendaji wa TASAF kijijini hapo hivi karibuni
 Bibi Zainabu Magali mnufaika wa mpango wa TASAF kunusuru kaya maskini akiwa mbele y nyumba yake aliyojenga kutokana na mpango huo. Wakati wa ziara ya kikao kazi baina ya wahariri, waandishi wa habari na watendaji wa TASAF iliyofanywa katika kijiji cha Ulongoni A hivi karibuni
Muhariri mwandamizi wa EFM radio na TV, Schola Mazura akimkabidhi kijana Salum Abdalla Pandu fedha zilizochangwa na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali waliokuwa wakishiriki kikao kazi Kati yao na watendaji wa TASAF walipotembelea kijiji cha Lubungo A na kumkuta kijana huyo ambae ni mjukuu wa mmoja ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini akieleza kushindwa kwake kukamilisha mchakato wa kupata mkopo kutokana na ukosefu wa fedha licha ya kupata ufaulu wa daraja la tatu katika mitihani ya kidato cha sita mwaka 2020.

WANUFAIKA wa  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF wa kusaidia kaya maskini nchini wameuomba mfuko huo kuendelea kuwasaidia kwani mbali na kuwanufaisha kwa mambo mbali mbali bado wanamahitaji ambayo TASAF ndio pekee wanaweza kuwakomboa.

Wanufaika hao kutoka kijiji cha Ulongoni A Morogoro wameeleza hayo wakati wahariri na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari walipotembelea kijiji hicho katika kukamilisha ziara ya kikao  kazi baina ya wahariri hao na watendaji wa TASAF.

Mmoja kati ya wanufaika hao, Tabia Gombe mkazi wa kijiji cha Ulongoni A amesema, mfuko wa TASAF umekuwa msaada mkubwa sana kwake,  umemsaidia vya kutosha, kwani pindi tu alipokuwa anapata fedh hizo alikuwa akizigawanya ambapo zilimuwezesha kusomesha watoto huku fedha nyingine wakitumia kununua mabati kidogo kidogo mpaka yamefikia kumi sasa.

Amesema, mabati hayo yatamuwezesha kuezeka nyumba yake  ili naye aweze kuishi mahali salama.

Amesema mwanzoni wakati mfuko huo unaanza alikuwa akipata Sh. 48,000/_  halafu baadae akawa anapata Sh.40,000 kisha ikaja 36,000 na sasa wanapata 32,000.

"Nawashukuru sana TASAF kwa msaada wao kwani sasa nalima mpaka Mbaazi die meongeza kuwa fedha hizo zimeniwezesha kupata uwezo wa kulima zao la Mbaazi linalotiwezesha kupata chakula na wajukuu zangu.


Naye Hawa Hamisi mmoja wa wanufaika mfuko huo wa TASAF amesema, mfuko huo umemsaidia Tasaf wajukuu zake ingawa bahati mbaya wengine wamekuwa akipata matokeo mabaya lakini hajaja tamaa na nashukuru TASAF nao wanaendelea kuwajali.

Nimeweza kuanzisha biashara ya kuku lakini walikuwa wanakufa pindi ugonjwa ukiingia, nilikuwa nanunua dawa lakini kumbe zingine zilikuwa ni feki na kuku walikuwa wanazidi kuendelea kufa... nilikuwa na kuku takribani 50 ambapo niliweza kiwasomesha wajuku zangu na kuwapatia mahitaji yote ya shule.

Kwa upande wake mume wa Hawa, Said Kakwamba  ameishukuru sana TASAF kwa kuwasaidia ila mpaka sasa bado wanahitaji msaada wao. "Tumesomesh wanafunzi, tumenunua kuku ila changamoto yake ni kufa tu. Ila hatukati tamaa..., Mpango wa TASAF. ni muhimu sana", amesema Kakwambwa.

Aidha ameupongeza mpango wa TASAF kwa kuwakabidhi Wakina mama Ruzuku na siyo  wababa kwani mwanzoni wakina baba walikuwa kwenyempango huu, lakini wengine walikuwa wakorofi, wengine wanywaji wa pombe na hata kama hanywi pombe kuchukua hela zile na hata kuongeza mke mwingine, ambapo mwanamke akiongea anaweza kupigwa na hata kufukuzwa.

Amesema lakini yeye na mke wake hawajawahi kufanya hivyo. Siri ya mafanikio tasaf imetuendeleza vizuri na wakiendelea kutusaidia itakuwa vizuri zaidi.

 Naye bibi Zainabu Magali ambaye ni mzee asiyekumbuka amezaliwa mwaka gani ila anasema wakati ule wa nzige alikuw mtoto  amesema mpango wa TASAF umemnufaisha kwani alikuwa na hali ngumu hakuwa na pa kuishi, nyumba ilikuwa kama analala nje, lakini mpango waTasaf ulipofika kijijini pale alipata fedha ambazo kwa kukutunza kidogo kidogo na kujihusisha na biashara ya kuku ambao anawauza kwa wasafiri barabarani alifanikiwa kujenga nyumba nzuri na kuezeka na bati na ndiyo anayoishi na kusomesh wajukuu zake huku akipata mahitaji yote ya shule.

"Kabla ya mpango huo hali ya maisha haikuwa nzuri kabisa, nilikuwa nalala kama niko nje nashukuru mpango huu umenisaidia, ninaishi na wajukuu sita ambapo mwanzo walikuwa kwenye mpango lakini sasa umebaki mmoja baada ya wengine kumaliza masomo na kutolewa kwenye mpango". amesema bibi magali.


Aidha TASAF wamesema wako kwenye mpango wa kuanzisha mpango wa ajira za muda kwa vijana wenye nguvu lakini bahati mbaya wanafeli masomo yao, tutawasaidia kupata ajira za muda ili waweze kujikwamua kiuchumi 

 Kwa upande wake Edna anayeishi kijiji cha Mkambalani amesema, mpango wa TASAF kusaidia kaya maskini umekuwa mkombozi kwa wengi, vijijini, na msaada wao huo bado unahitajika zaidi na zaidi.

Amesema, kupitia elimu waliyopewa na TASAF ameweza kuanzisha kikundi cha watu 25 ambao kwa pamoja wamekuwa na mradi wa sabuni ambazo wanauza n fedha zikipatikana wanakopeshana mankujiinua kiuchumi.


TASAF imeniwezesha kuanzisha biashara ya karanga ambapo watoto wangu watatu wako katika shule za bweni na mwaka huu wawili wanamaliza kidato cha nne na mwingine yuko darasa la sita. 

Amesema, baada ya Korona watoto walirudi chini kimasomo wakawa hawana ufanisi, shule zikaamuru wapelekwe bweni. Lakini kwa kutumia mpango wa Tasaf niliweza kuuza kuku zangu na watoto nikawalipia ada ya bweni.

Amesema, wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa katika kazi ya kuelimisha watu kuhusu mpango wa mfuko huo, lakini baada ya elimu sana sasa wameelewa na sasa katika kikundi 25 chetu tunakopeshana sabuni  na tunakopeshana hela kwa riba kidogo sana. Amesema, Tasaf wamepa uwezo mkubwa ambapo sasa kama ikitokea Tasaf wakamwambia apishe na aingie mtu mwingine kwenye mpango huo yuko tayari kwani ameishapatiwa elimuya kutosha kuweza kujiendeleza

Tunawashukuru sana Tassaf na wale wote walioamua mradi huu uje kwa watu kama sisi, mungu awabariki sana

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad