Spika
wa Bunge, Job Ndugai leo Agosti 26, 2020 ametangazwa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) Kupitia msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kongwa kupita bila kupingwa katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la
Kongwa.
Akitangaza matokeo hayo kwenye ofisi ya Halmashauri ya
wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Omary
Nkullo amesema Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Ndugai
ndiye pekee aliyekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
na kumfanya kupita bila kupingwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa
kuwa amepita bila kupingwa, Mheshimiwa Ndugai amesema anawashukuru wana
CCM, viongozi na wanachama kwa ujumla kwa heshima waliyompatia na
kumwezesha kupita bila kupingwa.
“Nahaidi kila haina ya
ushirikiano kwa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kongwa na kuhakikisha uchaguzi wa Jimbo la Kongwa unaenda vizuri, kwa
amani na salama”alisema Spika Ndugai
Pia, Mheshimiwa Ndugai ameahidi kuwa ataendelea kuwa mtumishi wa wanaKongwa na kuwa mwakilishi wao katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment