Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene, akimwangalia mtoto wa Kirundi alipokuwa anacheza
ngoma ya asili ya nchini Burundi, kabla ya Waziri huyo hajazungumza na
Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma, leo.
Simbachawene amefuta utaratibu uliokua umewekwa kwa wakimbizi nchini
pindi wanapokamatwa kutopelekwa mahakamani badala yake warudishwe nchini
kwao, hivyo kuanzia sasa mkimbizi yeyote atakayekutwa na makosa
atapelekwa mahakamani kisha jela endapo atakutwa na makosa ya kihalifu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene, akizungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu,
Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma, leo, ambao wanasubiri kupanda mabasi
kurudishwa nchini kwao kwa hiari. Amewapongeza Wakimbizi hao kwa kufanya
maamuzi ya busara kurudi nchini kwao kwasababu sasa nchi hiyo inja
amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:
Post a Comment