HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 18, 2020

Siku 14 Wenye Madeni kukatiwa Umeme

 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 kwa wateja wote wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wenye malimbikizo ya bili za Umeme kuhakikisha wanalipa madeni yao ama kusitishiwa huduma baada ya muda huo kupita. 


Waziri Kalemani ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Miradi na kazi mbalimbali za Umeme Jijini Arusha.


“Tunadai bilioni 69.7 kwa watu binafsi na bilioni 307 kwa Taasisi za Umma wote niwasihi kulipa Ankara za Umeme, hatutaki kupokea simu kulalamika, tunataka kupokea malipo” alisema Waziri Kalemani 

 Waziri Kalemani aliongeza kuwa TANESCO ni Shirika la kibiashara ambalo linajiendesha kwa mapato yake bila kutegemea ruzuku ya Serikali hivyo kuchelewesha malipo ya Ankara za Umeme ni kuchelewesha juhudi za Shirika hilo kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi kwa huduma bora na za Nishati ya umeme ya uhakika.


“Wananchi Wote, awe mtu binafsi, Taasisi za Umma, Wanaodaiwa ankara za Umeme, natoa siku 14 kuanzia Agost 17, waanze kulipia madeni yao, vinginevyo nawaelekeza TANESCO kuanza kukata Umeme, Meneja yeyote asipokata tutamkata yeye kwenye kazi” Mhe. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani 

Dkt. Kalemani aliendelea kwa kusisitiza Wateja wote wakiwemo Wateja binafsi na Taasisi za Kiserekali kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati kwani muda wa kusitisha huduma kwa wasiolipa ukifika, TANESCO na Wizara hawatasikiliza wala kupokea simu za maelezo ya mdaiwa sugu yeyote yule isipokuwa kusitisha huduma ya Umeme mpaka deni litakapolipwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad