Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Idara ya Mashirika yasiyo ya
Kiserikali Musa Leitura akiwaonesha mwongozo wa uratibu wa Mashirika
yasiyo ya Kiserikali washiriki wa kikao cha viongozi wa Mashirika hayo
Mkoani Kigoma.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Samwel Tenga akizungumza na viongozi wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kigoma.
Baadhi
ya viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kigoma
wakimsikiliza Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Samwel Tenga (hayupo
pichani) wakati wa kikao cha pamoja na viongozi hao.
Mwanasheria kutoka Idara ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya
Kiserikali Derek Mwajombe akitoa elimu kuhusu Sheria mpya ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2019 kwa viongozo wa Mashirika hayo Mkoani
Kigoma.
Picha zote na Idara ya Mawasiliano Serikalini
Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yametakiwa kutoa taarifa za kazi zao
kwa jamii ili kutimiza lengo lake la kuisaidia Serikali kutekeleza
miradi ya kuhudumia wananchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma , Samwel Tenga
wakati wa kikao cha pamoja na Mashirika hayo na timu ya ufuatiliaji
kutoka Ofisì ya Msajili wa NGOS.
Amesema lengo kuu la kuanzisha Mashirika siyo tu kujitafutia ajira lakini ni kuangalia pengo lililopo katika kuhudumia wananchi.
"Lengo ni kuangalia pengo ili kuhudumia wananchi, kuna Mashirika
ambayo yanapata ufadhili lakini changamoto ni mawasiliano kati ya
Mashirika hayo na Serikali ngazi ya Halmashauri hadi Mkoa kutokuwa
mazuri" alisisitiza
Amesema kwa uzoefu wa Mkoa wa Kigoma mawasiliano yamekuwa siyo mazuri
kwani kati ya Mashirika 150 yanayotambuliwa, yanayotoa taarifa si zaidi
ya Mashirika 10.
"Ni changamoto kwa sababu Serikali ya Mkoa au Wilaya inatakiwa ijue
Wadau wake na mchango wake kwa wananchi, kuna suala la kutoa taarifa za
miradi inayotekelezwa ila umekuwa na pengo la kutoa taarifa" alisema.
Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Mwandamizi kutoka Ofisi
ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Musa Leitura amesema
Serikali inatambua mchango wa Mashirika katika kuhudumia wananchi.
"Tumetembelea baadhi ya Mashirika, tumekuta miradi inaridhisha, kwa
maana hiyo tunatambua mnafanya kazi kubwa kuisaidia Serikali" alisema.
Ameongeza kuwa baadhi ya mapungufu yaliyobainika katika kufuatilia
mashirika hayo ni kutokuwa na Ofisi, kutowasilisha taarifa kwa Msajili,
kutokuwa na mpango wa uendelevu wa mradi na kutolipa ada.
Aidha, ameyasisitiza Mashirika kuzingatia sheria ili kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake na katika kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma Msafiri
Mzunusi amesisitiza Mashirika kushirikisha Serikali kuhusu mipango yake
kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi.
Naye Mmmjaya wadau wa NGOs Mkoani Kigoma Limbu Peter
ameishukuruOfisi ya Msajili wa NGOs kwa zoezi la ufuatiliaji
lililosaidia kubaini changamoto mbalimbali, hivyo kuzitatua na kusonga
mbele.
"Tunawashukuru sana kwa kupambanua masuala mengine ambayo tulikuwa hatuyafahamu ikiwemo suala la uendelevu wa miradi" alisema.
No comments:
Post a Comment