HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 12, 2020

NDIKILO -JAMII IZIDI KUTOA USHIRIKIANO KUFICHUA WAINGIZAJI DAWA ZA KULEVYA NA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA DAWA HIZO

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema hatua ya Serikali ya awamu ya tano kuanzisha Tume ya kupambana na dawa za kulevya na kuwezesha Kliniki ya tiba ya waraibu  Wilayani Bagamoyo inakwenda kuwa muarubaini wa vita dhidi ya mapambano hayo .

Ameeleza, waingizaji wa madawa hayo hawana nafasi kwa kipindi hiki na amewataka wananchi wazidi kutoa ushirikiano katika kutokomeza biashara hii kwa kuwataja majina ya wahusika wote ili vyombo vya Dola viwashughulikie.

Hayo aliyaeleza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa  miradi ya maendelo na kusikiliza kero za wananchi Wilayani Bagamoyo, ambapo alitembelea na kukagua ukarabati wa jengo la kliniki hiyo  iliyopo hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.

Akizungumza na  Waraibu mjini Bagamoyo, Ndikilo alieleza Serikali imefanya jambo jema kwa kuanzisha Kliniki hii ambayo kwa kiasi kikubwa imeweza  kuwasaidia Vijana ambao walijiingiza katika matumizi ya madawa hayo. 

Aidha alipongeza kwa mpango wa kuanzisha kliniki nyingine  ya waraibu katika Hospitali ya Mkoa ya Tumbi. 

Ndikilo alisema, waraibu hao kuachana na dawa za kulevya “Dawa za kulevya  sasa basi, dawa za kulevya ni hatari, yanaangamiza utu wa binadamu, yanaua nguvu kazi ya nchi Hongereni kwa uamuzi mliochukua kuachana na madawa hayo" alisema Ndikilo.

Alisema kwamba, Rais Dkt. John Magufuli tangu aingie madarakani ameendelea kupambana na dawa za kulevya na kuunda Tume ya kudhibiti dawa za kulevya Nchini.

"Juhudi zetu zimefanikiwa kupambana na dawa hizi, nipongeze Jeshi la Polisi kwa kupambana na hili, lakini bado ongezeni nguvu na taarifa  nazopata za kuripoti uwepo dawa za kulevya Mkoani Pwani zimepungua”alifafanua Ndikilo. 

Mkuu wa Mkoa  huyo aliwashauri waraibu hao, kutengeneza  vikundi vya ujasiriliamali ambavyo vitaweza kuwasaidia katika kuinua uchumi wao na kujishughulisha kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad