Mbeya City yavuna udhamini wa Milion 270 kutoka Parimatch - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 28, 2020

Mbeya City yavuna udhamini wa Milion 270 kutoka Parimatch

Klabu ya Mbeya City imevuna mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch Tanzania.

Mkataba huo unaanza rasmi msimu wa 2020/21 na una thamani ya zaidi ya milioni 270 za Kitanzania.

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana amesema anafurahi kuona kampuni yake inaendelea kuinua michezo ndani ya Tanzania.

Maligana amesema, ndani ya miaka mitatu Parimatch imeendesha programu mbalimbali za kuinua michezo Tanzania kama Amsha ndoto na leo ni hatua nyingine wanaifanya katika kukuza michezo.

Amesema, leo wameingia rasmi makubaliano ya mkataba wa udhamini wa Klabu ya Jiji la Mbeya ‘Mbeya City’, ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu huu wa 2020/2021.

"Mkataba huu ni wenye faida pande zote mbili ,mbeya City ni moja klabu kubwa kwa hapa Tanzania hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na ushawishi katika soka," 

Sisi kama Parimatch Moja ya jukumu letu kubwa ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya kimataifa ," amesema Maligana.

Ameongezea kuwa, Parimatch wataendelea na michakato mablimbali ya kuunga mkono vilabu vingine kutoka ligi kuu , ligi daraja la kwanza na hata Vilabu Chipukizi . Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na bodi ya ligi kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa.
Nae kiongozi wa Mbeya City ameishukuru Kampuni ya Parimatch kwa kuwapa udhamini ambao utaongeza chachu katika kikosi chao katika msimu wa 2020/21.
Mwisho , amewashuuru sana wadau wote wa soka nchini , kuanzia TFF , Bodi ya Michezo , Mbeya City - kuwa kuwapokea kuwa wadau rasmi wa michezo Ahsanteni Sana.


Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana ( wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makubaliano ya mkataba wa udhamini dhidi ya Parimatch na Mbeya City wenye thamani ya Milioni 270 kwa mwaka mmoja. Kushoto ni Kiongozi wa Mbeya City Emmanuel Kimbe. Juu wakiwa katika picha ya pamoja


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad