HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 19, 2020

KAMPUNI YA BIMA YA UAP YATOA VIFAAVYA KUKABILIANA NA CORONA KATIKA SHULE YA ENJAMINI MKAPA

 Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo akikabidhi matenki maalumu kwaajili ya kuoshea mikono kwa Afisa elimu taaluma Mkoa wa Dar es Salaam, Boniphace Wilson katika hafla iliyofanyika jana katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Dar es Salaam.Kulia ni Mkuu wa Shule ya Minazi Mirefu, Aveline Chugulu.Msaada huo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya utoaji wa huduma za bima Afrika Mashariki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo akipeana mkono na Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Benjamini Mkapa, Maliki Salum wakati Kampuni hiyo ilipokabidhi matanki 40 ya kuoshea mikono kwaajili ya shule za Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia (mwenye miwani) ni Mkuu wa Shule ya Minazi Mirefu, Aveline Chugulu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya UAP, Stephen Lokonyo akionyesha mfano jinsi ya kuosha mikono kwa maji na sabuni kutumia matanki maalumu ya kuoshea mikono yaliyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya Shule za Sekondari na Msingi za Mkoa wa Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika jana katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa.Kulia ni Afisa Elimu Taaluma Mkoa, Boniphace Wilson.Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Uenice Mganga.

Kampuni ya UAP Insurance Tanzania yachangia matanki kwaajili ya Shule za umma mkoa wa Dar es Salaam.

Katika kuadhimisha miaka 100 ya utoaji huduma kwenye soko la bima, Kampuni ya UAP Insurance Tanzania imetoa msaada wa matanki 40 ya kuoshea mikono kwaajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Matenki hayo yatasiaida kuhakikisha wanafunzi wanapata nafasi ya kunawa mikono yao kwa maji safi na sabuni hivyo kuhakikisha mazingira salama kwa Watoto shuleni. Kampuni hiyo ni kampuni tanzu ya kampuni ya UAP Holdings Plc inayotimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1920.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji kwa jamii na umelenga kuhakikisha wanafunzi wanakuwa kwenye mazingira salama wakati wote wawapo shuleni na kupunguza hatari ya kupata magonjwa.

“Tunafarijika kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau wengine katika kuhakikisha kwamba wanafunzi ambao ni taifa la kesho wanapata elimu bora. Msaada huu utahakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu katika mazingira ambayo ni salama kwa afya zao muda wote,” alisema.

Matanki hayo yatasambazwa kwenye shule za Msingi na Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam kulingana na mahitaji kama itakavyoelekezwa na Ofisi ya Elimu mkoa.

Akipokea msaada huo, Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Dar es Salaam,Boniphace Wilson alipongeza hatua hiyo akisema kwamba itasaidia kuongeza kasi ya udhibiti wa milipuko ya magonjwa mashuleni na kufanya mazingira ya kujifunzia kuwa salama zaidi.

“Tunawapongeza UAP Tanzania kwa kuona umuhimu wa kutoa matanki haya kwaajili ya shule zetu za Mkoa wa Dar es Salaam, hii itasaidia kuhakikisha wanafunzi wanapata nafasi ya kuosha mikono yao kwa maji safi na sabuni na kuleta usalama wa mazingira ya kujifunzia,” alisema.

 Msaada huo ni utekelezaji wa sera ya uwajibikaji kwa jamii ambayo UAP imekuwa ikiendesha katika maeneo mbalimbali ikiwamo Afya, elimu pamoja na mazinigira tangu ilipoanza kutoa huduma hapa Tanzania.


Kwa sasa kampuni hiyo inatoa huduma katika nchi mbalimbali ikiwamo Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad