HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 28, 2020

HUDUMA ZA EMIRATES ZAREJEA KWA MIJI 77 ZAIDI

SHIRIKA La ndege la kimataifa la Emirates limeendelea kufungua anga katika Miji mbalimbali duniani ikiwemo Afrika ikiwa ni sehemu ya kutoa huduma za safari ambazo zilisimama kufuatia mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, (Covid-19.)

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeelezwa kuwa, huduma katika miji ya Conakry, Guinea na Dakar, Senegal zimerejeshwa na zitaanza rasmi  Septemba 3 mwaka huu, na hii itafanya idadi ya miji ambayo inahudumiwa na shirika hilo barani Afrika kufikia nane.

Taarifa hiyo imeelezwa kuwa safari kutoka Dubai kwenda Conakry na Dakar zitakua mara mbili kwa wiki kupitia Boeing 777-300ER.

Aidha imeelezwa kuwa kupanuka kwa mtandao huo wa anga kupeleka ongezeko la kufikia miji 77 zaidi inayohudumiwa na Shirika hilo la kimataifa katika safari za anga.

Aidha shirika hilo limeendelea kuunganisha watu kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo kutoka Mashariki ya kati, Ulaya, Afrika, Amerika, na Mashariki ya kati kupitia Dubai na hiyo ni kutokana na huduma zao ambazo huwawezesha wateja kuweka machaguo yao ya safari kupitia shirika hilo au mawakala wake.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa baada ya Mji wa Dubai kufunguliwa kwa shughuli za biashara za kimataifa na utalii wateja wanaweza kuutembelea na wakiwasili suala la kupima Covid-19 ni lazima kwa wasafiri wanaowasili Dubai na UAE wakiwemo raia wa UAE na watalii bila kujali nchi walizotoka.

Imeelezwa kuwa sehemu zote zinazopendwa kutembelewa Dubai zikiwemo fukwe mbalimbali, sehemu za michezo na maonesho mbalimbali tayari zimefunguliwa na watalii kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni wanaweza kuzitembelea.

Ikumbukwe kuwa Dubai ni moja ya sehemu inayopendwa kutembelewa na watu wengi duniani, na kwa mwaka 2019 mji huo ulikaribisha wageni milioni 16.7 ambao waliunganishwa na Emirates, Shirika la ndege ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad