WATAFUNAJI
 watakao bainika kufuja fedha za walio katika mpango wa TASAF kipindi 
cha pili cha Awamu ya  Tatu unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii 
TASAF wameonywa kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo
 hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mfuko wa
 Maendeleo ya Jamii- TASAF, (National Steering Committee )  Eng. Rogatus
 Mativila, wakati wa kufuatilia zoezi la Uhakiki lililoanza leo kwenye 
Kata sita (6) Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza
 na Waandishi wa habari, Matavila, amesema kuwa kumekuwepo na Walenga 
hewa sio jambo jema hata kidogo jambo ambalo limekuwa likitolewa 
malalamiko sana.
“Uwepo
 wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji  aibu sana kwa viongozi wa 
mikoa, wilaya na Halmashauri.Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu 
yeyote. Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo 
ya vipimo nnitakavyotumia kujua kama mastahili kuendelea na nafasi 
mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio ukweli’’ Amesema Mativila.
Amesema
 katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, walengwa wa mpango wa 
kunusuru kaya maskini watahakikiwa kwa kuondolewa au kuingizwa katika 
mpango kwa kufuata vigezo vilivyowekwa a serikali.
Mativila,
 amesema kuwa Uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu ni muhimu katika 
kusimamia zoezi la uhakiki wa Walengwa wa  Mpango wa TASAF ambao  
utasaidia kupata Takwimu sahihi  za wanufaika Halisi  ndani ya Manispaa 
ya Morogoro.
Amesema 
 kuwa, Mkazo mkubwa katika Kipindi cha Pili utawekwa katika kuwezesha 
Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato 
na kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa  na 
kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na 
afya. 
Aidha,
 amesema Pamoja na hayo tathimini ya serikali ya utekelezaji wa TASAF 
kipindi cha kwanza awamu ya tatu inaonyesha umaskini nchini umepunngua 
kwa asilimia 10 kwa mahitaji ya msingi na umaskini uliokithiri umepungua
 kwa asilimia 12 kwa kaya maskini sana nchini.
 Amewasisitiza 
 Viongozi na Maafisa Waandikishaji Kaya kufanya kazi kwa uadilifu na 
weredi wakati wa utekelezaji wa Zoezi hili  kama maagizo yaliivyotolewa 
na Mh Rais katika hotuba  yake wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili 
kuhusu uwepo wa kaya hewa.
 “
 Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa 
viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri. Nitoe wito kwa wahusika wote 
kusimamia vizuri mradi huu. Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote.
 Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya 
vipimo nitakavyotumia kujua kama mnastahili kuendelea na nafasi 
mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio ukweli.” Amesema Mativila
Hata
 hivyo amewakumbusha  wananchi wote kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari
 wa COVID-19  ili   kuepuka Mikusanyiko isiyoyalazima, kuvaa barakoa,  
kuepuka kushikana  mikono na  kunawa mikono kwa sabuni kwa kutumia maji 
safi yanayotiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono.
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment