Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimuonesha mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck Ramani ya mkoa wake baada ya kumkabidhi
wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Shinyanga jana.Kulia ni Kamishna Msaidizi
wa Ardhi Usimamizi na Uratibu Wizara ya Ardhi Wilson Luge
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia hati ya
Bibi Zainab Kechuba kabla ya kumkabidhi
wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Shinyanga jana. Kushoto ni
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Hati miliki
ya ardhi Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi ofisi za ardhi mkoa wa Shinyanga
ambapo alizitaka taasisi za serikali kuhakikisha zinapima maeneo yao na
kumilikishwa. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck (Kushoto)
na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kuelekea kuzindua ofidi ya ardhi
mkoa jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikata utepe
kuashiria kuzinduliwa rasmi ofisi ya ardhi mkoa wa Shinyanga jana. Wa pili kulia
ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck akimuonesha samani Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa
wa Shinyanga Ezekiel Kitilya (Kushoto) wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa
wa Shinyanga jana. Kushoto kwa Waziri Lukuvi ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta
Mboneko.(PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA
WIZARA YA ARDHI).
========== ======= =========
Na Munir Shemweta, WANMM SHINYANGA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi William Lukuvi amesema zaidi ya wamiliki wa ardhi laki tisa nchini
hawajamilikishwa ardhi na kupatiwa hati na hivyo kuisababishia serikali
kushindwa kukusanya takriban bilioni 125.
Kufuatia hali hiyo Lukuvi ameagiza
wamiliki wote nchini wakowemo zaidi ya 60,000 wa mkoa wa Shinyanga ambao
viwanja vyao vimepimwa na michoro yake kuidhinishwa waende
ofisi za ardhi katika halmashauri za
wilaya kufuatilia hati ili waweze kumilikishwa ndani ya siku tisini
Waziri Lukuvi alisema hayo tarehe 3
Julai 2020 mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi ofisi za ardhi mkoa ikiwa ni
mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini.
Alibainisha kuwa, mwananchi ambaye
atashindwa kwenda kufuarilia hati yake katika kipindi cha siku tisini
atapelekewa stakabadhi ya malipo ikimtaka alipe kuanzia pale ambapo kiwanja
chake kilipimwa na michoro kuidhinisha.
"wale wamiliki ambao
watashindwa kufuatilia hati katika kipindi cha siku tisini wataanza kudaiwa
kodi ya pango la ardhi kuanzia pale michoro ilipoidhinishwa hata kama michoro
hiyo iliidhishwa mwaka 1962 ataanza kudaiwa kuanzia hapo maana itakuwa ni
uzembe wake" alisema Lukuvi
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi,
serikali inataka kila mtanzania apate hati miliki ya ardhi kwa mujibu wa sheria
kwa kuwa serikali inashindwa kukusanya kodi ya ardhi kwa mtu ambaye hana hati
na kuwataka wamiliki wachukue hati zao ili serikali ipate mapato na kutoa
huduma katika sekta mbalimbali kama vile barabara, maji na hospitali.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Zainab Telack alishukuru kuanzishwa ofisi ya ardhi mkoa wa shinyanga
na kueleza kuwa tayari amenza kuaona matunda ya ofisi hiyo kwa kupungua kwa
migogoro ya ardhi katika mkoa wake na kuwahimiza wananchi wake kwenda katika
ofisi za ardhi mkoa kuchukua hati.
"" kama mkoa tutahakikisha
tunaleta utulivu kutokana na kuanzishwa ofisi za ardhi katika mkoa wa shinyanga
kwa kuwa migogoro itakuwa imepungua"" alisema Zainab
Tayari zoezi la uzinduzi ofisi za
ardhi katika mikoa mbalimbali limefanyika katika mikoa kumi na linaendelea katika
mikoa ya Mara, Geita, Kagera, Lindi na Ruvuma.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi William Lukuvi Lukuvi aliwakabidhi hati za ardhi
wananchi pamoja na taasisi za serikali zilizopo mkoa wa Shinyanga akiwemo Bibi
wa miaka 77 Zainab Kechuba aliyeonesha furaha kubwa baada ya kukabidhiwa hati
yake.
Bibi Zainab alieleza kuwa, aliihangaikia hati
yake kwa muda mrefu lakini sasa amefurahi kwa kupatiwa hati yake na kumuombea
Rais John Pombe Magufuli umri mrefu na kuendelea kutawala Tanzania.
Waziri wa Ardhi alisema
mwaka huu uwe mwisho wa migogoro ya ardhi kwa kuwa huduma za ardhi zimepelekwa
karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa zenye wataalamu wa
fani zote za ardhi sambamba na kusambaza vifaa mbalimbali vikiwemo vya upimaji
katika mikoa.
No comments:
Post a Comment