HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 10, 2020

Ufungaji wa Midaki (Scanner) kubwa ya kisasa Afrika inayotumia mionzi kukagua mizigo inayopita bandari ya DSM, waridhisha



Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam,
Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali imeridhishwa na kasi ya ufungaji wa Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika katika bandari ya Dar Es Salaam inayotumia mionzi kukagua mizigo.
Mradi huo upo chini ya Wizara ya Nishati ambao unasimamiwa na kutekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia ngazi ya manunuzi: Ujenzi wa jengo la Midaki hiyo umekamilika kwa 99%, kazi ya usimikaji na ufungaji wa vifaa imekamilika kwa 51%, ambapo inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2020, kwa gharama ya zaidi ya Dola za kimarekani milioni 5, zikiwemo na fedha za kitanzania. 
Hayo yameelezwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati,Adam Zuber, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo,ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, walipofanya zaira ya kukagua maendeleo ya ufungaji wa midaki hiyo katika bandari ya Dar es salaam, Julai 7,2020.
Zuber alisema kuwa midaki hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kukagua magari makubwa ya mizigo mia mbili kwa saa, hivyo karahisisha utendaji kazi katika bandari hiyo na kuwatoa huduma kwa haraka kwa wateja.
Midaki hii itakuwa na uwezo wa kubaini aina mbalimbali za mizigo inayongia na kutoka nje ya nchi kupitia bandari hiyo, kuondoa udanganyifu uliokuwa unafanya na baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu waliokuwa wakipitisha bidhaa tofauti na zile zilizoelezwa katika nyaraka husika.
Alisema kuwa midaki hiyo pia,itaongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya ukusanyaji mapato ya serikali kwa kuwa itakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kukagua kila kitu kilichomo katika shehena ya mzigo ili ilipiwe kodi stahiki.
“Hii Midaki(scanner) ni muhimu sana kwa taifa letu, itarahisisha ukusanyaji wa mapato, kubaini kilichobebwa ndani ya gari, na kusafirisha mizigo kwa haraka zaidi, kimsingi kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wake,na tunaipongeza sana TPDC kwa kazi nzuri,hii ni midaki(Scanner) kubwa na ya kisasa kwa nchi za Afrika,”alisema Zuber.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, aliwahakikishia watanzania kuwa anaimani midaki hiyo itakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kwa kuwa asilimia kubwa ya utekelezaji wa mradi huo imekamilika.
Vilevile alieleza kuwa, midaki hizo mpya zitazotumia teknolojia ya  kisasa zitaboresha ukusanyaji wa mapato serikalini na kurahisisha utendaji kazi katika kukagua mizigo mingi itakayokuwa ikipita kwa wakati mmoja na kwa haraka zaidi.
“Mionzi iliyopo katika midaki hii haitakuwa na madhara kwa watumiaji kwa sababu wakandarasi wanaoijenga wamezingatia na kufuata sharia na taratibu za afya na usalama sehemu za kazi, hivyo nawatoa hofu watu wote juu ya hili, kuwa hakutakuwa na hatari zozote za kiafya kwa watumiaji,” alisema Dkt. Mataragio.
Naye Meneja wa mradi huo, Mjiofizikia Asiadi Mrutu wa TPDC ,alisema kuwa mbali na ujenzi wa midaki hiyo, pia wataboresha mifumo ya utendaji kazi katika bandari zote nchini, viwanja vya ndege,pamoja na kuondoa shehena za mizigo zilizopo mipakani.
Aliweka wazi kuwa wanufaika wa mradi huo unaofadhiliwa na  AfDB ni Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) na Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB).
Wengine ni Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu( PURA),Baraza la Uwezeshaji la Taifa( NEEC ), Mamlaka ya Huduma za Nishati na Mafuta Zanzibar(ZURA), pamoja na Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato Zanzibar( TRA-ZANZIBAR.) 
 Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakiwa katika picha ya pamoja walipofanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua ya mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kamshina wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, Adam Zuber, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio(pili kulia) na Meneja  mradi huo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli( TPDC), Mjiofizikia Asiadi Mrutu(kulia).
 Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakipata maelezo ya ufanyaji kazi wa Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, walipofanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kamshina wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati, Adam Zuber.
 Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakitoka kukagua maendeleo ujenzi na ufungaji Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, walipofanya ziara hiyo Julai 9,2020.
 Msimamizi wa ujenzi na ufungaji wa midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika Bandari ya Dar Es Salaam,Mhandisi Joseph Raymond (kulia) akitoa maelezo ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo kwa Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,walipofanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.
 Moja ya midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, ilivyoonekana wakati wa ziara Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC) unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,waliyoifanya ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.
 Jengo la kuendeshea mitambo na udhibiti midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika Bandari ya Dar Es Salaam, lilivyoonekana wakati wa ziara Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC) unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,waliyoifanya ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.
 Jengo la midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, lililokamilika kwa zaidi ya 90% lilivyoonekana wakati wa ziara Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC) unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,waliyoifanya ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.
 Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakiwa katika kikao cha mwisho wa mwaka wa fedha 2019/2020 kabla ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inaypita katika bandari ya Dar Es Salaam, Julai 9,2020.
Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said,(kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati,Adam Zuber,(kulia)wakipitia nyaraka za mkutano wa mwisho wa mwaka wa kamati hiyo kabla ya kufanya zaira ya kukagua maendeleo ya ufungaji wa midaki hiyo katika bandari ya Dar es salaam, Julai 7,2020.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad