HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 30, 2020

TANZANIA YACHUKUWA UENYEKITI WA NCHI 79 ZA OACPS NA KUELEZEA KIPAUMBELE CHAKE

Tanzania imesema itatumia kipindi chake cha uenyeketi wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific na Umoja wa nchi za Ulaya katika kusisitiza juu ya urejeshwaji wa rasilimali zilizoporwa katika nchi hizo nyakati za ukoloni,kuheshimu mamlaka ya nchi husika na urejeshwaji wa wahamiaji haramu kwa kuzingatia utu na haki za binadamu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. damas Ndumbaro ameyasema hayo wakati akishiriki mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya ya nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (OACPS) ambapo Tanzania inapata heshima ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi ya Balozi na Waziri katika nchi 79 za jumuiya hiyo.

Ameongeza kuwa mbali na masuala hayo pia Tanzania katika kipindi chake cha uenyekiti itatilia mkazo zaidi suala la mashirikiano ya kiuchumi ili kuziwezesha nchi zote za Jumuiya ya Afrika,Caribbean na Pacific kuingia katika uchumi wa kati ili kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi wake jambo litakalosaidia kupunguza uhamiaji haramu na kupunguza uhalifu wa kimataifa miongoni mwa nchi hizo.

Aidha amesema kuwa hoja nyingine ni kuhusu majadiliano yanayoendelea hivi sasa kati ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific na Jumuiya ya Ulaya ya kupata mkataba mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wa Kotonu uwe ni mkataba wenye manufaa kwa pande zote mbili utakaokuwa na msukumo katika suala la maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad