RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAZISHI YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA, LUPASO, MASASI MKOANI MTWARA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 29, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAZISHI YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA, LUPASO, MASASI MKOANI MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa kuelekea eneo la Makaburi kwa ajili ya Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja Wananchi wa Lupaso waliohudhuria katika Mazishi hayo ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa Lupaso Masasi mkoani Mtwara.
Mabregedia Jenerali wa JWTZ wakishuhudia Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa likishushwa kaburini Lupaso Masasi mkoani Mtwara.
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad