Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina
Ngalula (kushoto) wakiushukuru Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Horace Hui (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo wa TICTS, Donald Talawa kwa mchango wao wa kukabidhi msaada
wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.milioni 182, ikiwa ni
jitihada ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya afya,Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania
katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Horace Hui (wa pili kulia)
akizungumza na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi (wa pili
kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vya kujikinga na
ugonjwa wa Corona, vilivyotolewa na Kampuni hiyo, mwishoni mwa wiki
jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula (kushoto) pamoja na
Mkurugenzi wa Maendeleo wa TICTS, Donald Talawa.
Picha ya pamoja
====== ========= ======== ===============
KAMPUNI ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS),imetoa
msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.milioni 182, ikiwa
ni jitihada ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya afya .
Akizungumza
mwishoni mwai wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada
huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Mkurugenzi wa
Uendeshaji Donald Talawa amesema kuwa TICTS ni sehemu ya watanzania,
hivyo inawajibu wa kuunga mkono Serikali katika nyanja mbalimbali.
Talawa
amesema kutokana na Serikali kuongeza vituo vya afya, kampuni hiyo
imeona kuna umuhimu wa kusaidia vifaa mbalimbali vitavyosaidia vituo vya
afya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Talawa
ametaja vifaa hivyo walivyokabidhi kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni vitanda 100 ,mashuka, mito, vitakasa
mikono ambavyo serikali itapeleka katika vituo vya afya.
"TICTS
ni kampuni binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo ni sehemu ya
watanzania wa kuweza kuhakikisha tunaunga jitihada za Serikali katika
sekta ya afya kwa vifaa Kinfa na Tiba kutokana na kuongezeka kwa vituo
vya afya nchi nzima,"amesema Talawa.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi ameishukuru
TPSF kwa uratibu wao kwa sekta binafsi ikiwemo Kampuni ya TICTS
kuchangia vifaa tiba hivyo ili vituo vya afya kuwa na vifaa muhimu vya
kutolea huduma
“Wizara
ya afya pamoja na TAMISEMI kwa kipindi cha miaka mitano tumeimarisha
upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa kinga,hivyo tunaishukuru sekta
binafsi kwa kukubali kuchangia kwa umoja wenu katika jitihada za
serikali ili vituo vya afya kuwa na vifaa tiba,”amesema.
Aidha,
Prof. Makubi amesema kuwa Serikali inahakikisha vituo vya kutolea
huduma za afya nchini vinakuwa na vifaa muhimu vya kutolea huduma na
huduma bora zinazotolewa kwa wananchi pamoja na huduma zipatazo 13 za
kipaumbele ikiwemo huduma za mama na mtoto kwa kupunguzavifo vya mama na
mtoto.
"Sisi kama watumishi wenu tunathamini michango yenu,kwakweli mmefanya kazi kubwa".
Prof.
Makubi ameongeza kwamba kwa kipindi cha miaka mitano Serikali
imeongeza vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 7014 hadi 8783 ambapo
kuna ongezeko la vituo 1769 zikiwemo zahanati 1198 na vituo vya afya
487 na hivyo wataendelea kuimarisha upatikanaji wa vitaa tiba na dawa.
No comments:
Post a Comment