HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2020

Promosheni ya ‘TAJIRIKA NA eGazeti’ yazinduliwa jijini Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akizungumza na mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Mshindi huyo amejipatika kitita cha Sh1 milioni. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akionyesha namba ya mshindi wa kwanza wa Sh1milioni katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akizungumza katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai(kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela(kushoto) na aliyeko katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga wakiwa katika uzinduzi wa
wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

=====   =====   =====
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na pia watoa huduma kupitia njia mbalimbali za mtandaoni, imezindua rasmi promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendani wa MCL, Francis Nanai, alisema kuwa, promosheni hiyo inalenga kuwazawadia wasomaji wake, ambao kwa muda mrefu wamekuwa nao tangu kuanzishwa kwa magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya MCL hadi sasa ambapo unaweza kuyasoma magazeti mtandaoni kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Promosheni hii inakuja wakati ambapo,huduma ya kusoma magazeti mtaandaoni iliyopewa jina la eGazeti ikiwa na miezi mitatu lakini kwa muda mchache tu ina watumiajia zaidi ya 70,000 ndani na nje ya Nchi.

eGAZETI ni mfumo bora wa kusoma magazeti mtandaoni ya Mwananchi Communications Limited (MCL). Ili uweze kusoma magazeti mtandaoni unachotakiwa kufanya ni kupakua App ya eGazeti kwenye Google Playstore au tembelea www.egezeti.co.tz .

Kwa kutumia mfumo wa eGazeti unayasoma magazeti kutokwa Mwananchi Communications Ltd kwa urahisi na kwa bei nafuu ikiwemo kifurushi cha Shilingi1, 000 tu ambacho unasoma nakala ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.

Gazeti linapatikana kuanzia saa sita usiku, njia rahisi za kulipia gazeti, kuchangua vifurushi mbalimbali kadri ya uhitaji wako na eGazeti inakuwezesha kusoma machapisho hata kama utakuwa ‘offline’ baada ya kupakua mwanzoni, pia itakuwezesha kuona maktaba yako ambayo inakurahisishia usomaji.

Zaidi Ndugu Nanani alisema kuwa Tanzania ni nchi kubwa na kwakutumia Tehama na wabunifu wa hapa hapa ndani ya nchini wameweza kufanikisha eGazeti na kuwawezesha watanzania kusoma nakala zao popote walipo ambapo mitando inapatikana. Alisisitiza kila seketa inajukumu la kuwezesha vipaji na wao kama MCL wanafanya hivyo na HabariHub.

Dau Technologies nikampuni ya kiTanzania iliyo tumia fursa za HabariHub na kuweza kubuni na kuboresha mfumo wa kusambaza magazeti kwa njia ya mtandano.

“Tuna wasisitiza na ku”Promote” vijana wa kitanzania kuwa wabunifu na kutumia Tekenohama kufanya mapinduzi ya uchumi, hivyo tutaweza kujenga Taifa letu kuwa imara Zaidi” alisema Mr. Nanani.

Ndani ya eGazeti utaweza kuchagua na kulipia gazeti kwa: malipo kwa siku, malipo kwa wiki, malipo kwa mwezi, malipo kwa miezi mitatu na malipo kwa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Mhariri Mtendaji mkuu wa MCL, Bakari Machumu alisisitiza kuwa, lengo la MCL ni kuhakikisha kuwa wasomaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti wanapata habari zilizo bora na zinazokwenda na wakati na pia zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina.

Pia Mkuu wa Idara ya biashara wa MCL, Kenneth Mugabe alisema, katika promosheni hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zawadi za kila siku, wiki na za mwisho wa promosheni.

Zaidi ya milioni 100 zitashindaniwa. Milioni 20 kila mwezi, milioni 5 kila wiki na Milioni 2 kila siku, Na kubwa kuliko ni 20,000,000/= atakayoondoka nayo mshindi wa jumla katika droo kubwa ya mwisho wa promosheni baada ya miezi mitatu.

Droo za kila wiki zitakuwa zinarushwa kupitia chaneli ya YouTube ya Mwananchi Digital kila Jumanne saa nne kamili asubuhi kuanzia tarehe 07 June 2020. Katika promosheni hiyo itakayofanyika kwa wiki 12 mfululizo katika mikoa yote ya Tanzania, msomaji atatakiwa kununua na Kusoma magazeti ya Mwananchi, The Citizen and Mwanaspoti mtandaoni kupitia eGazeti kadri awezavyo.

Ili uweze kusoma magazeti piga 150*48# au Pakua App ya eGazeti kwenye Google playstore pia waweza kusoma kwa kutembelea tofuti yetu ya www.egazeti.co.tz.

Pointi ni jumla ya tokeni ulizoingiza katika droo baada ya kunua na kusoma magazeti. Kadri unavyoongeza pointi, ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda Vigezo na masharti vizitazingatiwa katika droo ya kutafuta washindi chini ya usimamizi wa na Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.

Machumu aliwataka watanzania kuchangamkia fursa kupitia promosheni hii na kusisitiza watu kufatilia na kushiriki maongezi kwenye mitandao yetu ya kijamii kupitia hashtags #TajirikaNaeGazeti pamoja na #SomaNaUshinde.
Mr Mugabe alimaliza kwa kutaja gharama za kampeni nzima hii Tajirika na eGazeti kuwa ni shilingi milioni mia mbili (200,000,000/=).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad