HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 27, 2020

BRAC YATOA V IFAA VYA KUNAWA MIKONO KWA SHULE ZA WILAYA YA TEMEKE

 Shirika la maendeleo la BRAC Tanzania limeunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zaa kuhamasisha usafishaji mikono kwa kutoa msaada wa vifaa vya kusafisha mikono katika jiji la Dar es Salaam.



Mchango huo ulitolewa kwa Maafisa wa wilaya ya Temeke ikiwemo Afisa wa Elimu wa wilaya (jina), Afisa wa Afya wa wilaya (jina) na Mkurugenzi wa wilaya (jina) na ulijumuisha sabuni ya maji na idadi ya vifaa vya kusafisha mikono vitakavyogawiwa kwa shule za Wilaya ya Temeke.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa BRAC nchi Tanzania Fordson Kafweku amesema kuwa BRAC kama shirika lilijokita katika maendeleo ya jamii lina jukumu la kuunga mkono Serikali na jamii kwa ujumla pale ambapo kunakuwa na uhitaji. Tangu kuzuka kwa ugonjwa unaoenezwa na virusi vya korona, Serikali imekuwa ikihamasisha usafi na haswa kujenga tabia ya usafi wa mikono kwa kunawa mara kwa mara kutumia maji tiririka na sabuni. 

"Tunajivunia kuweza kushirikiana na Serikali kwa kutoa mchango huu leo kwa shule za Wilaya ya Temeke hasa katika kipindi hiki ambapo shule zinakaribia kufunguliwa tena. Zoezi la kunawa mikono mara kwa mara ni tabia ambayo inabidi kujengeka katika jamii yetu kwa sababu sio tu inaweza kuzuia kuenea kwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya korona bali magonjwa mengine mengi, "amesema Kafweku.



"Tangu mlipuko wa ugonjwa wa korona, kipaumbele chetu cha kwanza kilikuwa ni kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu kwa kuhakikisha tuwapa elimu ya kujikinga ikiwa ni pamoja na utgawaji wa vifaa kinga kama barakoa, vitakasa mikono na glavu wanapokuwa wanapoendelea kutekeleza majukumu yao. Hata hivyo, tumekuwa pia kwenye mstari wa mbele wa kusambaza elimu na hatua za kinga kwa umma kwa kutumia njia mbalimbali za vyombo vya habari, "Kafweku.


BRAC imekuwa ikitoa elimu kupitia kurasa zake za kijamii, pia kwa kusambaza vipeperushi kwa jamii na kuwasiliana na wanajamii wakiwemo wateja na washiriki wa program za BRAC kupitia njia ya simu na meseji ambapo wananchi zaidi ya milioni 2.5 wamefikiwa na taarifa hizi. 

BRAC maendeleo Tanzania kwa sasa inatekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa elimu ya makuzi na malezi kwa watoto wadogo wa Play Lab Play unaotekelezwa jijini Dar es Salaam na Mbeya na miradi ya mbali mbali ya uwezeshaji vijana inayolenga wasichana inayotekelezwa katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.

BRAC pia iko katika hatua za mwsho za kukabidhi sabuni na vifaa vya unawaji mikono 24 katika mkoa wa Tanga ikiwa ni pamoja na halmashauri ya jiji la Tanga na wilaya ya Korogwe na vifaa vingine 12 vitatolewa katika shule za mkoa wa Mbeya. Thamani ya vifaa vyote vitakavyokabidhiwa katika mikoa hii ni TZS 14,100,000. 

Aidha, shirika hilo hivi karibuni lilikabidhi sabuni na ndoo 99 za kuosha mikono kwa ofisi za serikali za mitaa katika maeneo ya Temeke na Vingunguti jijini Dar es Salaam, vile vile mkoani Tanga na Mbeya.
Mkurugenzi wa BRAC Maendeleo Tanzania, Fordson Kafweku akinawa mikono baada ya kuwakabidhi Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kukabidhi kwa shule za Manispaa hiyo, BRAC wameunga jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zaa kuhamasisha usafishaji mikono kwa kutoa msaada wa vifaa vya kusafisha mikono katika jiji la Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo J. Mwakabibi akinawa mikono baada ya kukabidhiwa vifaa na sabuni kutoka Shirika la maendeleo la BRAC Tanzania ambapo wameunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zaa kuhamasisha usafishaji mikono kwa kutoa msaada wa vifaa vya kusafisha mikono katika jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo J. Mwakabibi akizungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru Shirika la Maendeleo BRAC  Tanzania baada ya kukabidhiwa vifaa vya kunawia mikono.
Mkurugenzi wa BRAC Maendeleo Tanzania, Fordson Kafweku (pichani mbele kulia) akikabidhi vifaa vya unawaji mikono na sabuni 14 kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo J. Mwakabibi (pichani kushoto). Vifaa hivyo vyenye thamani ya TZS 14,100,000/= vimekabidhiwa kwa ajili ya matumizi ya shule 14 zilizopo wilaya ya Temeke.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa vya kunawia mikono kutoka Shirika la Maendeleo BRAC Tanzania kwa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam

1 comment:

Post Bottom Ad