Absa Tanzania yawapa wateja ahueni - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 8, 2020

Absa Tanzania yawapa wateja ahueni

· Yatoa msamaha wa kulipa madeni kwa hii miezi mitatu


NA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

Benki ya Absa Tanzania imetoa msamaha wa malipo ya madeni kwa wateja wake katika kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed amesema msamaha huo ni kwa wateja wa rejareja, wafanyabiashara na makampuni na uwekezaji.

“Tumechukua hatua hii kwa kutambua athari za kifedha na kiuchumi zilizoikumba Tanzania na dunia nzima kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19,” alisema Mohamed.

Alisema programu hiyo ya ahueni katika ulipaji madeni ni ya miezi mitatu ikiambatana na jitihadi nyingine kadhaa za benki hiyo katika kupunguzia wateja athari walizokumbana nazo kutokana na janga la corona.

Mpango huo ulioanza tangu Aprili mwaka huu unafanyika kwa kufuata matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Tunatambua kuwa hiki ni kipindi kigumu kwa wateja wetu ambao mipango yao ya kifedha na biashara zao zimekumbana na athari hasi.

“Kwa hiyo sisi kama washirika wa tunaowajibika, tunafuraha kuwasapoti wateja wetu hawa na biashara zao ili kuendelea kujenga ustawi wa kibiashara na uchumi bora pamoja na kuwapo kwa changamoto za sasa.

“Tunawaomba wateja ambao hawajaathirika kuendelea kufanya malipo/marejesho kama kawaida. Hii itatuwezesha kupanua wigo wa kutoa unafauu kwa wengine wengi zaidi ambao huenda wanamahitaji makubwa. Wateja wetu wanahimiza kuwasiliana na mameneja uhusiano,” alisema Mohamed.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma Bora wa Wateja, Samuel Mkuyu, alisema upendo wa Absa kwa wateja wake umeimarika zaidi huku moyo wa kujitolea na kuwalinda haujayumba hata kidogo.

“Na hii ndio sababu huduma zetu zimeendelea kama kawaida huku zikiendana na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya. Tunawashauri wateja wetu kutumia huduma za kimtandao ambazo ufanisi wake umeimarika zaidi na ni salama katika mazingira tuliyonayo sasa,” alisema Mkuyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad