Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.
Godfrey Nyaisa amekabidhi vifaa vya Tehama kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji wa Mafinga, Bi. Saada Mwaruka kwa ajili ya utoaji wa Leseni za
Biashara kielektroniki katika Halmashauri hiyo.
Makabidhiano
hayo yamefanyika Mei 19, 2020, katika Ofisi za BRELA Makao Makuu Jijini
Dar es salaam yakishuhudiwa na Maofisa kutoka BRELA na Maofisa Biashara
kutoka katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Akizungumza
katika hafla fupi ya Makabidhiano Bw. Nyaisa ameeleza kuwa lengo kuu la
kushirikisha Halmashauri katika zoezi la utoaji Leseni kielektroniki ni
kutengeneza mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara.
“Mfumo
huu ni rahisi sana na unamuwezesha Mfanyabiashara kuweza kupata Leseni
akiwa popote pale. Mfumo huu utahitaji Mfanyabiashara aweze kuweka
viambatanisho vinavyotakiwa kisha ataweza kupata Leseni yake”.
Amebainisha Bw. Nyaisa.
Aidha
Mtendaji Mkuu ameeleza kwamba, katika hatua za awali mfumo huu unaweza
kuwa na changamoto kadhaa kwa Wafanyabiashara kutokana na matumizi ya
mtandao lakini anaamini wakipewa msaada wa karibu basi wataweza kuuzoea
mfumo huu mapema.
Amewataka
pia kuusimamia vizuri mfumo wa utoaji wa Leseni vizuri ili hata wakati
utakapofika wa Halmashauri zingine kuanza kutoa Leseni kuwa mfumo huo
basi ziweze kujifunza kutoka kwao.
Vifaa
vilivyokabidhiwa siku ya leo ni pamoja na Kompyuta za mezani tatu,
Kompyuta mpakato moja, tambaza (scanner) moja, Kichapishi (Printer)
moja, Modemu moja na Simu za Mkononi tatu.
Naye
Kaimu Mkuu wa Idara ya Leseni BRELA, Bw. Tawi Kilumile amebainisha
kwamba ili mfanya biashara aweze kuomba na kupata Leseni ya Biashara
kielektroniki inabidi atembelee tovuti ya www.Business.go.tz kisha
kutengeneza akaunti na kuandaa ombi lake la Leseni.
Aidha atatakiwa kuwa na nakala ya Hati ya Usajili wa Kampuni au Cheti cha kuandikisha Jina la Biashara.
Nakala
ya Katiba ya Kampuni (Memorandum & Articles of Association)
zinazoonesha majina ya wamiliki wa Kampuni, hisa wanazomiliki na saini
zao.
Nakala
ya Hati ya kuandikishwa kama mlipa kodi (TIN), nakala ya Mkataba wa
pango, nakala za Vitambulisho vya wenye hisa katika Kampuni.
Kibali/Hati/Leseni
kutoka kwenye Mamlaka za Udhibiti kwa biashara zinazodhibitiwa na
Mamlaka za Serikali (Wizara, Mamlaka, Idara, Taasisi au Wakala za
Serikali) cha kuruhusu kufanyika kwa biashara husika.
Vigezo hivyo vikiwa ni kwa Leseni itakayomilikiwa na Kampuni au Mtu/Watu wenye kumiliki Jina la Biashara.
Na
ikiwa mwenye biashara ni Mtu Binafsi basi atatakiwa kuwa na nakala za
Kitambulisho cha mwenye Biashara kama vile Pasi ya kusafiria,
Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mpiga kura au Cheti cha
kuzaliwa (kwa raia wa Tanzania), na kibali cha Kuishi Nchini kwa asiye
Mtanzania.
Nakala ya Hati ya kuandikishwa kama mlipa kodi (TIN).
Nakala
ya Mkataba wa pango au Hati ya Umiliki yenye jina lake. Nyaraka hizi
ni kwa ajili ya uthibitisho wa mahali biashara husika itakapokuwa
inafanyika
Akitoa
shukrani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga ameishukuru BRELA
kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kama ilivyo kusudiwa ili
kuweza kutimiza lengo la Serikali la kufikia uchumi wa Kati.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.
Godfrey Nyaisa (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,
Bi. Saada Mwaruka (kulia) pichani juu wakisaini Mkataba wa makabidhiano
ya ya vifaa ya Tehama kwa ajili ya utoaji wa Leseni kimtandao katika
Halmashauri hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika jana Mei 19, 2020,
katika Ofisi za BRELA Makao Makuu Jijini Dar es salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.
Godfrey Nyaisa (kulia) akimkabidhi Modemu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mji wa Mafinga, Bi. Saada Mwaruka (kushoto) kama ishara ya Makabidhiano
ya vifaa vya Tehama kwa ajili ya utoaji wa Leseni kimtandao katika
Halmashauri hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika Mei 19, 2020, katika
Ofisi za BRELA Makao Makuu Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment