HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 5, 2020

Absa Tanzania yaunga mkono juhudi za serikali mapambano dhidi ya Covid-19

Waziri wa Afya, Maendeleo ya. Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, (katikati), akimshukuru Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utumishi wa Benki ya AbsaTanzania, Patrick Foya (kushoto), baada yakupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuisaidia serikali katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona (Covid-19). kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mabula Daudi Mchembe. Vifaa hivyo vikiwemo barakoa, vitakasa mikono na gloves vyenye thamani ya shs milioni 20 vimekabidhiwa katika ofisi za wizara hiyo jijini Dar
es Salaam leo.

:Mkurugenzi Rasilimali watu na Utumishi wa Benki ya Absa TanzaniaPatrick Foya (kushoto), akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada
wa vifaa tiba kusaidia juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa
wa corona (Covid-19), kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya. Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati). kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof.
Mabula Daudi Mchembe.Vifaa hivyo vikiwemo barakoa, vitakasa mikono na
gloves vyenye thamani ya shs milioni 20 vimekabidhiwa katika ofisi za
wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya. Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu, akizungumza wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa Mkurugenzi
wa Rasiliamali Watu na Utumishi wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick
Foya (kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kusaidia juhudi
za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). Vifaa hivyo vikiwemo
barakoa, vitakasa mikono na gloves vyenye thamani ya shs milioni 20
vimekabidhiwa katika ofisi za wizara, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad