HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 7, 2020

WAZIRI UMMY MWALIMU AMKABIDHI RC MAKONDA VIFAA VYA KUNAWA MIKONO KWA AJILI YA KUWAKINGA WANANCHI NA CORONA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Vifaa mbalimbali 350 vya kutakasa Mikono Ikiwemo Ndoo za Maji, Madumu, Masks na Dawa za kuchanganya kwenye Maji kwaajili ya kuwakinga wananchi dhidi ya Vimelea wa Virusi vya Corona.

Akipokea Vifaa hivyo RC Makonda amesema atahakikisha Vitapelekwa sehemu mbalimbali ikiwemo Vituo vya Daladala, Masokoni na sehemu zenye mzunguko wa watu ili Wananchi waweze Kusafisha mikono kabla ya kufanya jambo lolote.

Aidha RC Makonda amewaelekeza Wakurugenzi wote wa Manispaa za Jiji hilo kuhakikisha Maji yenye Dawa hayamaliziki kwenye ndoo za kunawa mikono.

Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza Wananchi kuendelea Kuchukuwa tahadhari dhidhi ya Ugonjwa huo huku akiwaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa.

Msaada huo wa Vifaa 1,000 umetolewa na Mfanyabiashara Subash Patel chini ya Umoja wa Wafanyabiashara Wazawa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo kwa Dar es salaam wamekabidhi Vifaa 350 na Vifaa vingine 650 vilivyosalia vitasambazwa nchi nzima.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto MheUmmy Mwalimu akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Dar es salama matenki 1000 kwa niaba ya mikoa mingine kwa ajili ya wananchi kunawa mikono kujikinga na maambukizi ya COVID 19,Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda
Mkuu wa mkoa wa Dar es salama Mh Paul Makonda akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo jijini Dar,mara baada ya kukabidhiwa  matenki 1,000 kwa niaba ya mikoa mingine kwa ajili ya wananchi kunawa mikono kujikinga na maambukizi ya COVID 19.
Mfanyabiashara Subash Patel akizungumza jambo kwa niaba ya Umoja wa Wazalendo,Wafanyabiashara Wazawa,Mama Lishe na Wamachinga waliotoa msaada wa matenki 1000 kwa niaba ya mikoa mingine kwa ajili ya wananchi kunawa mikono kujikinga na maambukizi ya COVID 19,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo kwa Dar es salaam wamekabidhi Vifaa 350 na Vifaa vingine 650 vilivyosalia vitasambazwa nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad