HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 28, 2020

WANANCHI WAFURAHIA BARAKOA

WANANCHI wa Kijiji cha Mnyoma kata ya Mdimba wamemshukuru Afisa Tarafa Mambamba Prisca Sanga kwa kuwapatia Barakoa (vikinga pua na mdomo) pamoja na kupatiwa elimu ya matumizi yake.

Wananchi hao wamemshukuru Afisa Tarafa Prisca kwa kuwapatia Barakoa pamoja na elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi Corona. 

"Afisa Tarafa wetu ameonyesha njia kwa kutupatia Barakoa pamoja na elimu ya matumizi yake, tunamshukuru sana.  Tutaendelea kuvaa Barakoa, tutaendelea kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na njia nyinginezo za kujikinga na Covid 19. Tunaiunga mkono Serikali na kusikiliza ushauri wa Wataalamu wa afya katika kupambana na virusi vya Corona" alisema Mwanakijiji  Haidary Shetta.

Akizungumza mara baada ya kugawa Barakoa hizo, Afisa Tarafa Prisca aliwasihi Wananchi kuzingatia tahadhari zote za kujikinga na virusi Corona.

"Tarafa ya Mambamba tunapigana vilivyo dhidi ya ugonjwa Covid 19. Barakoa hizi ni sehemu ya mapambano ya vita dhidi ya virusi Corona. Tuendelee kusikiliza ushauri wa Wataalamu wa afya pamoja na kuzingatia maelekezo ya Serikali." Alisema Prisca Sanga, Afisa Tarafa Mambamba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad