Airtel Tanzania yachangia sh. 700 milioni kwa wafanyakazi wa sekta ya afya dhidi ya mapambano ya COVID-19 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 27, 2020

Airtel Tanzania yachangia sh. 700 milioni kwa wafanyakazi wa sekta ya afya dhidi ya mapambano ya COVID-19

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) alipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania, Gabriel Malata (kushoto) mfano wa hundi ya shilingi milioni saba (TZS 700,000,000) ukiwa ni mchango wa Airtel Tanzania kuunga mkono serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mapambano dhidi ya virusi vya covid-19 (corona). Mchango uliotolewa na Airtel utatumika kununua vifaa kinga vitakavyosambazwa nchi nzima ili vitumike na watoa huduma wa afya. Airtel inatoa msaada huu kwa mara nyingine ambapo awali ilishirikiana na wizara pia kwa kutoa uelewa kwa njia ya sms pamoja na kuboresha mawasiliano ya Intaneti bure kwa sehemu zilizotengwa kwaajili ya kutoa huduma kwa waathika wa virusi orona nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi wa Airtel Tanzania (hayupo pichani) mara baada ya Kukabidhi hundi ya shilingi Milioni mia saba (TZS 700,000,000) toka Airtel Tanzania kwaajili kusaidia juhudi za serikali kupitia wizara ya Afya kupambana na virusi vya Covid-19 (Corona) nchini. Waziri huyo alisema pesa hizo zitatumika kununua vifaaa kinga kwaajili ya watoa huduma wa Afya na vitasambazwa nchi nzima.
Mwenyekiti wa Bodi wa Airtel Tanzania Bw Gabriel Malata akiongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia saba (TZS 700,000,0000) kwaajili ya kusaidia serikali katika mapambano dhidi ya virusi ya covid-19 (corona) katikati ni Waziri wa Afya Bi Ummy Mwalimu na kulia ni Mganga Mkuu wa serikali Prof Abeli Makubi.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania leo imetoa kiasi cha Tzs 700,000,000 milioni (Milioni mia saba) kwa Wazira wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ikiwa ni kuunga mkono wafanyakazi wa sekta ya afya kwa mapambano dhidi ya COVID-19. Hatua hiyo imetangazwa leo wakati wa kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto. 

Hali ya usalama kwa wafanyakazi wa sekta wa afya walio kipaumbali dhidi ya mapambano dhidi ya COVID-19 imekuwa mashakani tangu kuibuka kwa virusi vya Corona hapa nchini kwa sababu ya kila siku kukumbana na wagonjwa walioambukizwa au wenye dalili za ugonjwa huo. Airtel Tanzania inatambua ya kuwa bila hatua za haraka kuchukuliwa kwa kuwapa vitendea kazi bora, wafanyakazi wa sekta ya afya watakuwa hatarini ya kuambukizwa virusi hivi na hivyo kupelekea wagonjwa kukosa watu wakuwapa tiba. Wafanyakazi hao wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira mangumu hivyo ni muhimu  kujikinga dhidi ya maambukizi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Gabriel Malata  alisema, ‘Napenda kuchukua nafasi kuipongeza serikali kwa kiasi kikubwa ambacho imeweza kuchukua kwa kupambana na virusi vya Corona tangu kisa cha kwanza kuripotiwa hapa nchini. Nawapongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa elimu ambayo wamekuwa wakitoa mara kwa mara kuhusu janga hili na kuweza kuwafanya Watanzania wachukue tahadhari kubwa juu ya kujikinga na hatimaye leo visa vya ugonjwa huu hapa nchini sio kubwa sana’.

Aliongeza,’Kama mnovyojua, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania Plc inamilikiwa na ubia baina ya Serikali na Bharti Airtel. Serikali inamiliki hisa asilimia 49 huku zingine zikimilikiwa na Airtel. Kwa sababu hiyo, ni vyema kutambua kuwa kampuni ya Airtel Tanzania Plc ni kampuni ya mawasiliano ya Watanzania.

Kwa kutambua hilo, sisi Airtel Tanzania Plc tunatambua umuhimu wa afya kwa Watanzania. Zaidi ni kwamba tunaona juhudi kubwa za serikali za kupambana na janga la Corona hapa nchini. Airtel Tanzania imeweza kuguzwa na hilo na hivyo kwa pamoja tumeamua tujitokeza na kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na janga hili na kwa leo tunatoa hundi yenye dhamani ya Tzs700,000,000 milioni (Milioni Mia Saba tu) kwa ajili ya vifaa tiba kwa wafanyakazi wa sekta ya afya. Tunaelewa kiasi hiki sio kikubwa sana lakini kitaweza kusaidia kupambana na janga hili kwa namna moja au nyingine. Tunaamini kuwa afya ya Watanzania ni moja ya nguzo muhimu kwa sisi Airtel kuendelea kukua kwetu hapa nchini’.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania George Mathen alisema, ‘Airtel Tanzania leo inatangaza kuchangia Tzs700,000,000 milioni (Milioni mia saba) dhidi ya mapambano ya COVID-19 hapa nchini Tanzania. Mchango huu unaelekezwa kwa wafanyakazi wa sekta ya afya walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Corona. Kwa sasa ni muda muafaka na sahihi kutumia uwezo wetu kuwasaidia manesi, madaktari pamoja na wafanyakazi wengine kwenye sekta ya afya. Kwenye janga hili, hakuna nchi ambayo inaweza kusimama na kupambana kivyake. Sekta binafsi ni muhimu kusimama pamoja na serikali dhidi ya kupambana na janga hili’.

Kwa upande wake Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu alisema, huu ni ushirikiano muhimu na Airtel Tanzania na hii inadhihirisha ni kwa kiasi ngani tunawapa kipaumbele wafanyakazi wa sekta ya afya ambao wako mbele kwenye mapambano dhidi ya COVID-19. Kwa sisi pamoja na jamii nzima ya Watanzania ni muhimu kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya kujikinga na janga hili la Corona.

Airtel tayari imechukua hatua kadhaa na hasa kwenye msongamano dhidi ya wateja wakati wa mlimpuko huu wa corona kwenye maduka yake yote nchini kwa kuwapa sanitiza na glovu za mkono kwa wafanyakazi wake wote. Kampuni ya Airtel vile vile imekuwa ikisambaza ujumbe mfupi wa maneno dhidi ya kujikinga na Corona kwa wateja wote wa Airtel bila gharama yoyote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad