HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 14, 2020

Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege yapewa elimu na TCRA

Afisa Masoko wa TCRA Dorice Muhimbila akimkabidhi zawadi mwalimu kutokana na kujibu swali  kwa usahihi.

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege wakisikiliza mada kutoka TCRA.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa katika matumizi ya mitandao kuacha kuweka vitu binafsi katika mitandao.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya  Wavulana Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani  Afisa Masoko wa Mamlaka hiyo  Dorice Muhimbila amesema kuwa Wanafunzi ni muhimu kuwa elimu hiyo ili wakianza kumiliki simu waweze kutumia mawasiliano hayo salama.

Muhimbila amesema kuwa elimu hiyo wanayoitoa ni kuelekea kilele cha maadhinisho ya Siku Walaji wa Huduma za Mawasiliano ambayo huadhimishwa kila Machi 15 ya Kila Mwaka

Amesema kuwa kuna sheria ya makosa mitandao hivyo wanafunzi wanatakiwa kupewa muongozo ili mwisho wa siku wasiweze kuangukukia katika mikono ya sheria wakati wa kutumia mawasiliano.

Muhimbila amesema kuwa TCRA imejipanga katika utoaji wa elimu katika makundi yote katika kuhakikisha wananchi wanatumia mawasiliano kwa usalama.

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Mwandamizi Robson Shaban amesema kuwa wanafunzi wakipata elimu wanakuwa mabalozi kwa jamii nzima.

Amesema katika kipindi hiki teknolojia ya mawasiliano inakua hali ambayo lazima iendane na utoaji  elimu.
Nae Mkuu wa Shule hiyo Enock Walter amesema kuwa elimu waliyoitoa katika Shule hiyo ni kubwa kwani hata walimu itawasadia katika utumiaji wa mawasiliano.

Aidha amesema TCRA waendelee kuwafikia mara kwa mara kuweza kupata elimu ya mawasiliano hasa kwa wanafunzi ambao ndio watarajiwa wa kutumia mawasiliano.


 Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Mwandamizi Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyosimamia mawasiliano pamoja na utoaji elimu.


 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege Enock Walter akizungumza namna walivyopokea elimu iliyotolewa na TCRA katika Shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad