MAKATIBU WAKUU : ZIARA HII NI YA KIPEKEE, TUMEJIFUNZA MENGI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 4, 2020

MAKATIBU WAKUU : ZIARA HII NI YA KIPEKEE, TUMEJIFUNZA MENGI


ZIARA ya makatibu wa wakuu na manaibu katibu wakuu imekuwa ni ya kipekee kwao kwani wamemkiri kuwa wamejifunza mengi ya kitaalamu na yasiyo ya kitaalamu, kwa kazi kubwa inayofanyika katika Mradi wa kujenga Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR).

Ziara ya siku mbili ya kutembelea mradi huo kutokea jijini Dodoma hadi jijini Dar es Salaam kwa kupita barabara maalumu ya kutengeneza Reli ya Kisasa ya (SGR) ili kuwawezesha makatibu na manaibu hao kuona kwa ukaribu ujenzi wa Reli hiyo.

Katika ziara hiyo makatibu wakuu walipita katika maeneo mbalimbali kutoka jijini Dodoma hadi Morogoro maeneo mojawapo ni Ihumwa Camp, Kikombo, katika eneo linalotengenezwa Mahandaki pamoja na katika kiwanda cha kutengeneza mataluma.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo, Katiu Mkuu wa wizara ya Katiba na sheria ambaye pia ni mwenyekiti wa ziara hiyo, profesa, Sifuni Mchome amesema kuwa kazi kubwa inayofanyika katika mradi huu katika maeneo mbalimbali, ambayo yameshakamilika.

"Tumeshuhudia kiwanda cha Mataluma, sehemu panapotengenezwa makaravati pia tumeona reli iliyokamilika pamoja na kuona jinsi wataalamu wanavyounganisha reli ili kusitokee mtikisiko wakati reli itakapoanza safari zake." 

"Sayansi na Teknolojia inayotumika ni ya Kisasa na niyahali ya juu kiasi kwamba hata sisi, inatuingiza katika tasinia nyingine ya watu ambao wanatumia reli ya kisasa na niyakisasa kweli, sio reli ya kubahatisha ya kuunga unga hapana". Amesema Prof. Mchome

Licha ya hilo Makatiu wakuu hao waliweza kupanda treni iliyowekwa kwaajili ya majaribio kwa maeneo ambayo yamekamilika mpaka sasa na kujionea vile inavyofanya kazi.

"Tumetembelea kutoka kituo kimoja kimoja mpaka kufika hapa soga tulikuwa tukisikiliza ile mitikisiko na hatukuona mtikisiko wa aina yeyote ikiwa na maana ni kweli ule uunganishaji kweli umefanyika kimakini.

"Kwasasa Tunatekeleza ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amazo aliahidi kweli tunatekeleza kwa maana kwama tunayaishi yale maisha ya watanzania, maisha ya kulisema jambo na kwenda kulifanya, na sio maisha ya kusema jambo na kuanza kuzunguka zunguka na kutoa visingizio". Amesema prof. Mcchome.

Amsema maisha haya ni ya kufanya kazi na kutekeleza kama nchini imeahidi kwa wananchi ikiwa na maana ya kodi za wananchi zinakwenda kufanya shughuli zilizolengwa.


Kwa upande wake katibu mkuu wa uchukuzi katika wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt.Leonard Chamuriho amesema kuwa kiwango cha reli ni kizuri na maendeleo yake ni mazuri.

"Leo makatiu wakuu wamekuja kujionea wenyewe maendeleo ya ujenzi wa reli hii, maeneo yaliyoaki ni maeneo korofi nayo mafundi wanaendelea kuyafanyia kazi hasa katika eneo la mto Mkondoa ndipo panachangamoto kubwa." Amesema Dkt. Chamoriho.

Hata hivyo amesema kuwa kilomita 15 wameweza kupanda Treni ya majaribio na kuona mwenendo wake na treni ya majaribio na kusafiri kwa starehe mpaka kufikia kituo cha soga.

Kwaupande wake Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni na michezo na msemaji mkuu wa serikali, Dkt. Hasan Abasi amesema kuwa unaweza kusafiri kwa starehe bila vinywaji wala simu kutikisika ukiwa katika treni ya majaribio.

"Watu wakae Mkao wa kula ili treni ikikamilika waweze kupanda au ukipenda unaweza ukanunua tiketi kabisa ukisubiri ikamilike tuu". Amesema Dkt. Abas
 Makatibu wakuu na naibu katibu wakuu wakiingia katika treni ya majaribio mara ya kuacha magari katika ziara ya simu mbili ya makatibu hao.
 Makatibu wakiwa katika Treni ya majaribio kujionea starehe watakayoipata mara baada ya kukamilika mradi wa reli ya kisasa utakapo kamilika.
 Moja ya picha ya gari lilokowa likitembea katika barabara inayotumika katika ujenzi wa reli ya kisasa ikiwa imepigwa na mpiga picha akiwa kwenye Treni ya majaribio.
 Muonekano wa Treni ya majaribio kwa ndani wakiwa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu.
 Mwonekan wa Reli ya kisasa iliyokamilika kwa kila kitu hadi nguzo za umeme.
 Hii ni stesheni ya Soga makatibu na manaibu wakiwa wameshika katika treni ya majaribio.
 Makatibu wakuu na manaiu wakiwa nje ya stesheni ya soga.

 Picha ya Pamoja ya makatibu wakuu na manaibu katika stesheni ya Soga iliyokamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad