DAWASA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUSHIRIKI UZALISHAJI MAJI CHANZO CHA RUVU CHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 8, 2020

DAWASA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUSHIRIKI UZALISHAJI MAJI CHANZO CHA RUVU CHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Mamlaka ya maji safi na Usafi Dar es Salaam na Pwani DAWASA kwa watendaji wanawake kuhusika katika uzalishaji wa maji.

Wanawake wa Dawasa wameshiriki katika uzalishaji maji katika chanzo cha maji cha Ruvu Chini.

Akizungumzia Siku ya wanawake ambayo huadhimishwa Machi 08 kila mwaka, Mkurugenzi wa Mahusiano na Jamii Dawasa , Neli Msuya amesema wameamua kushiriki maadhimisho hayo kwa kwenda chanzo cha Ruvu Chini ili kusaidia Uzalishaji wa maji.

Amesema, mwanamke ana mchango mkubwa sana katika jamii na lengo ni kumtua mama ndoo kichwani kama adhma ya kutimiza malengo ya Makamu wa Rais Samia Suluhu.

"Tumeamua kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki pamoja kwenye uzalishaji wa maji kwenye chanzo cha maji Ruvu Chini lengo likiwa ni kusaidia uzalishaji huo pamoja na kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais Samia Suluhu la kumtua mama Ndoo Kichwani," amesema.

Neli, amesema lengo la serikali ni kufikia asilimia 95 kwa mijini kufikia mwaka huu na kwa sasa Chanzo cha Ruvu Chini kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku ambapo ni zaidi ya asilimia 70 ya maji yanayozalishwa na Mamalaka hiyo.

Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini Dawasa Emaculata Paul amesema anafurahi kujumuika na wanawake wa Dawasa katika kushiriki uzalishaji mani na maji hayo yatatumika katika siku ya wanawake.

Amesema, wamedhamiria katika kumtua mama ndoo kichwani pamoja na wanawake waweze kushiriki katika maendeleo ya kiuchumi.

Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Bagamoyo, Judith Nginika amewashukuru wanawake kwa umoja kuweza kushiriki kwa pamoja katika kuzalisha maji kwenye mtambo wa Ruvi Chini ambapo ni Mkoa wake kihuduma.
Watendaji wanawake wa Mamlaka ya maji safi na Usafi Dar es Salaam na Pwani DAWASA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kazi ya uzalishaji maji katika chanzo cha maji cha Ruvu Chini, wanawake wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku
Mhandisi Lilian na Afisa habari wa Dawasa Everlasting Lyaro wakiwa wanasoma mita ya maji katika bomba la kusafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini, Wanawake watendaji wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku
Wanawake wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku
Wanawake watendaji wa Dawasa Rosemay Lyamuya(kulia)  na Neli Msuya wakiwa wakiwa kazini, wanawake wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini Dawasa Mhandisi Emaculata Paul(kulia) na 08 kila mwaka, Mkurugenzi wa Mahusiano na Jamii Dawasa , Neli Msuya wakiwa kikazi zaidi, wanawake watendaji wa   Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini Dawasa Mhandisi Emaculata Paul akizungumzia ushiriki wa wanawake watendaji wa Dawasa kushiriki katika uzalishaji maji, wanawake wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku.
Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Bagamoyo Judith Nginika akiwa anapima ubora wa maji katika maabara ya Mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini, wanawake wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku.
Mkurugenzi wa mahusiano na Jamii Dawasa , Neli Msuya akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ushiriki wao katika uzalishaji wa maji, Wanawake watendaji wa Dawasa waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushiriki uzalishaji maji kutoka chanzo hicho ambacho kinazalisha maji Lita Milion 270 kwa siku

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad