HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 30, 2020

WABUNIFU WA MAVAZI KUJIPANGA KULINDA MAZINGIRA.

TAMASHA la Sita la Mavazi ya Stara, STARA FASHION WEEK 2020 Linatazamiwa kufanyika tarehe 17 na 18 Jijijini Dar es salaam ikiwa ni wiki moja kabla ya kuupokea Mwezi Mtukufunwa Ramadhani. 

Tamasha hili la kila mwaka linatazamiwa kuwa na wabufu wapatao 30 huku likishirikisha wafanyabuashara na wajasiriamali mbalimbali kuuza bidhaa zao. 

Kwa mujibu wa waandaji wa tamasha hili kaulimbiu ya mwaka huu ni Fashion Katika kutunza Mazingira.

Akizungumza nasi Latifah Makau Mwanzilishi wa Stara Fashiion Week anasema  "Industry ya Fashion   inatajwa kuwa  msababishaji mkubwa wa uchafuzi wa mazingira duniani, na kwamba jukwaa hili la fashion lijulikanalo kama Stara limeona umuhimu wa kuhasisha wabunifu kufikiria nje ya box kwa kujipanga kuonyesha  uwezo wao kupitia Mabaki Mali.

Tunataka kuanzisha kampeni hii ya vita dhidi ya uchafuzi wa mazingirab kupita mitindo. Sawa na kuja na suluhisho ya nini kifanyike kupungiza takataka zizalishwazo na mafundi baada ya mavazi kushonwa.

Na kwamba  kauli mbiu ya Stara ambayo ni Eco Fashion  Mwaka huu itawaleta pamoja wabunifu katika harakati za vita dhidi ya uchafuzi huu wa mazingira lakini pia kuonyesha namna ambavyo mbunifu amaweza kujiongezea kipato kupitia mabaki anayozalisha. Lakini pia  watazamaji watashuhudia mavazi na mapambo yaliyobuniwa kwa muongo huo na hivyo watarajie burudani ya aina yake.  Hii ni katika  kuendeleza na kutambulusha mpango wa kuzalisha mali mpya kutokana na kauli mbiu yetu mabaki Mali, na hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Mkakati huu ni kelee za "wito wa kutaka hatua zichukiwe.” anasema Latifah.
Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako.


Hivyo tunapaswa tuwe makini katika kujenga mazingira yetu kwa sababu vitu vingine huyaharibu, kama vile uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa bahari, uchafuzi wa ardhi, n.k.

Tunapaswa kutunza mazingira yetu..

Uchafuzi wa mazingira unaweza kushughulikiwa kupitia aina mbalimbali sera za matumizi ya ardhi, mipango na mazoea ya usimamizi. Harakati kama hizi pia ni  pamoja nazo.

Uzinduzi wa msimu mpya wa STARA unatazamiwa kuchukua nafasi yake tarehe 29 Februari  katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam na baada ya hapo warsha na seminar mbalimbali zitaelekea kuelekea kilele cha Tamasha hilo.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad