KAJALA APATA UBALOZI WA TAULO ZA KIKE ZA RANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 3 January 2020

KAJALA APATA UBALOZI WA TAULO ZA KIKE ZA RANI

Muigizaji Frida Masanja 'Kajala' akiwa pamoja na Binti yake Paula wakionesha taulo za Kike za Rani baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Gerirwa General Suppliers


Muigizaji Frida Masanja maarufu kama Kajala amepata shavu la kuwa balozi wa taulo za kike  kutoka Kampuni ya Gerirwa kwa muda wa mwaka mmoja. 

Kampuni hiyo imempa ubalozi wa taulo za kike Kajala na binti yake Paula ambapo wameanzisha programu ya Binti Shuleni itakayolenga katika kuwasaidia wanafunzi wasioweza kuhudhuria shuleni wawapo kwenye hedhi kwa kuwapa msaada wa taulo hizo.

Shule zilizolengwa ni zile za Sekondari za serikali kwa mikoa yote Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa taulo hizo za kike na kusaini mkataba, Kajala amesema amefurahi kuteuliwa kuwa balozi na yeye kama mama anajua changamoto wanazozipata watoto wa kike kipindi cha hedhi hivyo atatoa elimu kwa mabinti.

"Ukiachana na mwanangu Paula mimi ni mama wa watoto wengi nazijua changamoto nashukuru kwa kunichagua na kuniamini nitafanya kazi vizuri mimi kama mama" Kajala.

Naye Paula ambaye ni mtoto wa Kajala  ameshiriki  katika tangazo la kuzielezea pedi hizo za Rani  ameambatana na mama yake katika uzinduzi huo na kushudia mama yake akisaini mkataba wa kuwa balozi kwa mwaka mmoja.

Paula ameishukuru kampuni ya Gerirwa kwa kumchagua na kumpa nafasi mama yake kuwa balozi na kutoa ushauri kwa wamama na mabinti kutumia pedi sahihi ambazo azitawaletea matatizo kama miwasho.

"Nimefurahi kuwa sehemu ya  tangazo nawashauri wamama na wasichana wenzangu watumie taulo hizo za kike kipindi chao cha hedhi" Paula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taulo hizo za kike  Hawa Hassan amesema kuwa wamemchagua Kajala kuwa balozi na wanampango wa kusaidia wanafunzi mashuleni ili kutatua changamoto wanayokutana nayo wakati wakiwa katika kipindi cha hedhi ikiwa kikiwa taulo za kike.

"Moja la lengo letu ni kusaidia ya changamoto ya watoto wa kike ambao wanashindwa kwenda shuleni kisa taulo za kike hivyo tutatoa msahada mashuleni na tutatoa katika shule za serikali ikiwa ni moja ya kuunga mkono juhudi za serikali yetu.

Kampuni hiyo imeanzishwa na Wanawake wawili ambao ni Hudaa Badi na Hawa Hassani.
 Muigizaji Frida Masanja 'Kajala' (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Rani Hawa Hassan wakitia saini makubaliano ya Ubalozi wa mwaka mmoja wa kutangaza taulo za Kike za Rani. Picha ya Chini wakionesha Mkataba huo 
 Muigizaji Frida Masanja 'Kajala' akikata utepe wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya Ubalozi wa mwaka mmoja wa kutangaza taulo za Kike za Rani. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Rani Hawa Hassan akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya Ubalozi wa Taulo za Kike kwa Muigizaji Frida Masanja 'Kajala'.

1 comment:

Post Bottom Ad