Timu ya taasisi ya Her Initiative wakifurahi pamoja wakati wakiwa katika maandalizi ya mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Panda kwa mwaka 2020, yatakayofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam. Zaidi ya wasichana 30 kutoka sehemu mbalimbali watashiriki katika mafunzo ya uundaji na utoaji huduma katika jamii zao ili waweze
kujikwamua kiuchumi.
Sehemu ya Majaji katika mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Panda kwa mwaka 2020 ambao pia ni washirika (partners) wakimfamfia usaili mmoja wa wasichana watakaoshiriki mafunzo hayo katika kipengele cha mradi (Mapambo, Uokaji keki na mapishi).
Na Diana Aggrey.
Kwa mara nyingine , taasisi ya Her Initiative imeratibu uendeshaji wa mradi wa Panda kwa mwaka 2020. Mradi huu wa Panda wenye lengo la kuwawezesha wasichana kati ya miaka 18-30 kufikia maendeleo ya kiuchumi, kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipengele vitano ambavyo ni Kilimo cha mbogamboga, Uokaji wa keki, Upishi,Mapambo na utengenezaji wa kucha ,pamoja na elimu ya kifedha,Utunzaji wa kumbukumbu elimu juu ya ukatili wa kijinsia,na usimamizi wa biashara. Zaidi ya wasichana 30 wanashiriki katika mradii huu wa Panda kwa kupata mafunzo ya uundaji na utoaji huduma katika jamii zao ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Lengo la mradi wa Panda ni kuwawezesha na kuwafundisha wasichana ujuzi mbalimbali na muongozo ili baada ya mafunzo waweze kujiajiri na baadae kuweza kuwaajiri wengine, lakini pia kupata usimamizi wa kimawazo katika biashara kwa walio watangulia kutokana na vipengele walivyochagua ili kuweza kuendesha biashara zao vizuri pindi watakapoanza.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Wasichana katika biashara kutumia fursa za mafunzo na ushauri ili kujiinua na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi binafsi".
Mradi huu wa panda ni wa miezi 10 na utaambatana na shughuli mbalimbali kama; mafunzo ya vitendo na nadharia, miezi mitatu ya usimamizi wa kimawazo kwa biashara zao, warsha itakayolenga kuwakutanisha wasichana wajasiriamali wachanga pamoja na sekta binafsi na za serikali zinazotoa mikopo na mitaji, kampeni ambayo itafanyika kwenye mitandao ya kijamii kuzungumzia changamoto pamoja na fursa kwa wasichana wajasiriamali.
Her Initiative inashirikiana na wadau na mashirika mbalimbali katika utoaji wa mafunzo haya wadau hawa ni; Women International First Fund,DOT,Lavy_Product,Mama peridot,Oasis Event, Manka_Cakes,Hedhi Cup,EFM,Reach and Save The Needy,Centum Learning. Tunakaribisha mashirika /Watu binafsi ama taasisi yoyote yenye lengo la kumuinua mtoto wa kike (Msichana) kiuchumi kuungana nasi katika kuendesha na kuendeleza mradii huu.
HER INITIATIVE ni shirika lisilo la kiserikali na si la kibiashara . Shirika hili limeanzishwa kwa lengo la kuwaelimisha wasichana katika jamii ili waweze kujitambua na kushiriki katika harakati zozote za jamii zinazohusu au kugusa maisha yao. Dhamira kuu ya shirika ikiwa ni kuwaelimisha na kuwapa wasichana kipaumbele , katika jamii ili kuchochea maendeleo ya usawa
No comments:
Post a Comment